- Binadamu

Lishe bora ni muhimu kwako na kwa familia yako

Sambaza chapisho hili

Kuna uhusiano mkubwa kati ya kile tunachokula, hali ya afya yetu na uwezo wa miili yetu kupambana na magonjwa na vimelea vinavyosababisha magonjwa.

Chakula bora kwa afya zetu na watu wanaotuzunguka ni muhimu kwa ajili ya kuendelea kuzalisha mali na kujenga jamii iliyo bora. Kuwa na afya njema, inatukumbusha wazalishaji wa mazao ya kilimo juu ya aina ya chakula tunachozalisha katika mashamba yetu, tunavyotumia nyumbani na kuuza kwenye soko.

Matokeo ya lishe duni ni pamoja na maambukizi ya mara kwa mara, kukosa nguvu ya kufanya kazi, watoto wanakuwa na hatari ya kupata utapia mlo, kuwa na uzito mdogo, na wale wanaokwenda shuleni wanashindwa kufanya vizuri. Hii inachangia kuwa na hali duni katika maisha kwa miaka yao ya baadaye.

Katika makala hii, tunaangazia mikakati kadha wa kadha ambayo unaweza kutumia nyumbani ili kuhakikisha kuwa familia yako inajengwa na kudumishwa vyema.

Mlo kamili kwa ajili ya lishe ya binadamu

Ni nini mahitaji ya lishe kwa familia

Makundi tofauti katika familia yana mahitaji tofauti ya lishe. Hii inategemea umri, kazi na viungo mwilini, na aina ya shughuli wanazoshiriki. Katika familia, kuna makundi yafuatayo;

  • Wanawake wajawazito,
  • Wamama wanaonyonyesha
  • Watoto wachanga miezi 0-6
  • Watoto miezi 6-23
  • Vijana – kuanzia kubalehe
  • Watu wazima – wanaofanya kazi
  • Wazee / wakongwe

Panga chakula kulingana na mahitaji ya lishe ya makundi haya. Hakikisha kila mtu anapata lishe ipasavyo hasa wale ambao hawawezi kujitunza.

Ikiwa hawatashughulikiwa, afya zao zitaharibika na wataathiriwa zaidi na magonjwa kwani kinga yao inakua chini. (Tutazingatia mahitaji ya kila kikundi katika toleo lijalo la MkM la mwezi Julai).

Lishe na vyanzo vya kawaida vya chakula

Lishe bora inajumuisha aina ya vyakula kutoka kwa makundi tofauti ya chakula, na hutoa virutubisho na ladha tofauti tofauti.

Makundi hayo ni pamoja na;

  1. Nafaka, mizizi – mahindi, viazi, ndizi – Wanga, kuongeza nguvu
  2. Mikunde – maharagwe, soya – Protini ya kujenga mwili
  3. Karanga, mbegu – Njugu, korosho – Protini ya kujenga mwili
  4. Maziwa – ya ng’ombe, mbuzi – Protini ya kujenga mwili
  5. Mayai – ya kuku, bata – Protini ya kuenga mwili.
  6. Nyama – ng’ombe, kuku, samaki – Protini ya kujenga mwili
  7. Matunda na mboga rangi ya chungwa, njano – karoti, malenge – Vitamini A kuongeza kinga
  8. Mboga ya kijani kibichi – kunde, managu, mchicha – Madini chuma (Iron) ya undaaji wa damu.
  9. Mboga zingine – nyanya, kitunguu, kabegi – Vitamini na madini kwa ajili ya kuzuia maambukizo.
  10. Matunda mengine – Parachichi, mananasi – Vitamini na madini kwa ajili ya kuzuia maambukizo.

Hakikisha chakula chako kina makundi ya msingi ya kuongeza nguvu (wanga), kujenga (protini), kuongeza kinga (vitamini na madini). Hivi ni vikundi vya msingi na hutoa virutubisho muhimu kwa maisha na ukuaji. Tumia vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika eneo lako.

MUHIMU: Zingatia usafi wa hali ya juu katima mfumo mzima wa utayarishaji wa chakula.

Zalisha chakula kuzingatia makundi ya chakula

Zalisha vyakula vya aina tofauti ili kukidhi mahitaji ya lishe ya familia yako. Tumia aina ya mazao inayoambatana na hali ya hewa ya eneo lako na mbegu yenye ubora wa hali ya juu. Usilime tu au kufuga kwa ajili ya soko au biashara.

Tafuta habari ya kuongeza maarifa juu ya mbinu na teknologia za uzalishaji wa chakula ambayo yanahakikisha lishe bora.

Hifadhi maji, rutuba ya udongo, ambayo huongeza uzalishaji wa kilimo kwa muda mrefu. Usifungue shamba kwa kuchoma, na utumie mabaki ya mazao kama lishe ya wanyama au mbolea.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *