Kabla ya kusindika maziwa ya mgando au mabichi ni lazima kufanya vipimo vya awali ili kujua kama maziwa yanafaa kusindika au hayafai. Kipimo kikubwa kinachotumika kupima maziwa ni alkoholi (Ethanol) Kipimo hiki hutumika kutambua maziwa yaliyoharibika na maziwa yaliyoanza kuganda. Namna ya kupima Chukua kiwango kinacholingana cha Alkoholi (ethanol) na maziwa mabichi kisha changanya pamoja kwa kuweka katika chombo maalum…
Usindikaji
Unaweza kusindika ngozi kiasili kupata bidhaa bora
Usindikaji wa viwandani unahitaji mitambo mikubwa, maeneo makubwa nguvu kazi kubwa, malighafi nyingi. Hivyo inahitaji mtaji mkubwa. Njia hii pia inahitaji kemikali za viwandani hivyo sio rafiki kwa mazingira. Usindikaji wa asili ni rahisi kwani malighafi za uchakataji hupatikana katika mazingira yanayotuzunguka. Njia hii inashauriwa sana kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana mitaji mikubwa na unaweza kuchakata ngozi moja kwa…
Usindikaji wa Mvinyo kwa matunda ya asili
Vijana wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kusindika mazao kutumia malighafi za hapa nchini. Mvinyo ni neno linalotokana na neno la kireno vinho, ni kinywaji kinacho tengenezwa kutokana na majimaji ya matunda mbalimbali. Kuna aina nyingi za mvinyo kufuatana na matunda yaliotumika. Katika Makala hii Mkulima Mbunifu inaangazia Kijana wa kike kutoka mkoani Mbeya alivyoamua kujitoa kimasomaso katika kusindika matunda kupata mvinyo…
Ufugaji wa samaki kibiashara ni njia rahisi yakuongeza kipato
Kumekuwa na mfumko wa watu wengi mijini na vijijini kuingia katika ufugaji wa samaki. Miradi hii huwagharimu fedha nyingi, lakini hufa baada ya muda mfupi. Ili mfugaji aweze kuwa na ufugaji wenye tija, hana budi kujifunza ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vifaa vingine vinavofanana na hivyo, vyenye uwezo wa…
Tahadhari za kuchukua nyakati za msimu wa mvua katika ufugaji samaki
Ufugaji wa samaki una kanuni na taratibu za kufuata ili kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa. Msimu wa masika ni muhimu kuufuatilia ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza. Katika makala hii Mkulima Mbunifu linakuangazia hatua muhimu za kuzingatia wakati wa masika ili kufanya ufugaji samaki wenye tija. Nyakati za msimu wa mvua ni vema kuzingatia hatua zifuatazo ili kuepuka madhara…
Utunzaji, uhifadhi na usafirishaji bora wa Maziwa
Ni muhimu kujua baadhi ya mambo ambayo husababisha maziwa kuharibika ili uweze kuzuia hasara zisizokuwa za lazima. Maziwa yana virutubisho vingi sana. Kwa sababu hiyo, bakteria waharibifu huweza kukua kwa haraka kwenye maziwa. Kwa wasafirishaji wa maziwa, nii muhimu kufahamu vyema jinsi maziwa yanavyoweza kuharibika haraka kama hayatatumika na kuhifadhiwa vizuri au hayatasafirishwa kwa haraka. Ni muhimu kuwa na uelewa…
Sindika Machungwa kuepuka hasara na upotevu usio wa lazima
Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa sana kwa wingi katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Mwanza. Zao hili ni la chakula na biashara. Ikiwa huu ni msimu wa machungwa, wakulima hawana budi kujifunza namna mbalimbali za kusindika zao hili ili kuondokana na upotevu unaotokana na wingi wake na kukosekana kwa soko…
Mkulima anaweza kujiongezea kipato kwa usindikaji wa ngozi
Ngozi hukaushwa ili kuzuia uharibifu unaotokana na kuoza kwa kuwa si ngozi zote zinazozalishwa hupelekwa kiwandani zikiwa mbichi ili kusindikwa. Ngozi zikioza hupoteza ubora wake na hivyo kutokuwa na manufaa katika matumizi mbalimbali. Ngozi ni zao la mifugo linaloweza kutoa mchango mkubwa kuwainua kiuchumi wafugaji na jamii kwa ujumla. Baadhi ya wajasiriamali hutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na ngozi ya ng’ombe,…
Jifunze kusindika nazi na kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali
Kusindika nazi Katika msimu huu, nazi zinapatikana kwa wingi mashambani na sokoni na hivyo kufanya gaharama za uuzaji kuwa chini kidogo. Hata hivyo pamoja na upatikanaji huu, wakulima na wauzaji wengi hawajafikiria namna ya kuongezea thamani zao hili ili kuzalisha bidhaa bora zaidi zenye soko na muda mrefu wa matumizi. Mkulima Mbunifi unashauri kusindika nazi na kuzalisha bidhaa hizo ili…
Unaweza kuongezea thamani Mtama kwa kuzalisha mvinyo
“Kwa karne nyingi, mtama umekuwa ukichukuliwa kama chakula cha watu maskini au chakula cha njaa, hili sasa limegeuka na kutoa matumaini mapya kwa wakulima wa mtama nchini Tanzania” Mtama ni kundi la mbegu ndogo ndogo aina ya mazao ya nafaka, yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe. Hii ni aina ya mazao yanayolimwa katika mazingira magumu kama…