- Usindikaji, Viazi vitamu

Jifunze njia rahisi ya kukausha viazi vitamu

Sambaza chapisho hili

Viazi vitamu ni moja ya mazao ya mizizi ambayo huvumilia ukame. Zao hili hulimwa karibu katika mikoa yote.

vitamu hasa vya rangi ya karoti vina virutubishi vya vitamini A kwa wingi ambavyo vinahitajika sana katika mwili.

Kulingana na uzalishaji mwingi ni muhimu kukausha viazi vitamu ili kuviongezea thamani, ubora na matumizi yake. Viazi vitamu husindikwa pia ili kupata viazi vilivyokaushwa, unga, wanga na jamu.

Kukausha viazi vitamu

Ukaushaji wa viazi vitamu hutumia nishati ya jua.

Kanuni muhimu za ukaushaji

  • Ukaushaji hupunguza maji kwenye zao la viazi vitamu ambayo yakiwepo husaidia ukuaji wa vimelea vya magonjwa na kusababisha kuoza. Ukaushaji hupunguza maji kwa kiasi kikubwa na kuwezesha hifadhi ya muda mrefu.
  • Ukaushaji utategemea hali ya unyevu hewani na hufanikiwa vizuri iwapo unyevu kwenye hewa ni mdogo. Viazivitamu vina vimeng’enyo ambavyo husababisha upotevu wa rangi, virutubishi na ladha wakati wa kukausha. Inashauriwa kuzuia hali hiyo kwa njia ya kuchemsha kidogo kabla ya kukausha.

Mambo ya kuzingatia katika ukaushaji bora wa viazi vitamu

  • Viazi vikatwe katika vipande vyenye unene, upana na urefu usiozidi sentimita 6. Ukubwa wa vipande ukizidi huo ulioshauriwa, ukaushaji huchukua muda mrefu na mara nyingi ubora wa bidhaa hushuka.
  • Tandaza viazi katika kina kilicholingana ili ukaukaji uwe kwa pamoja. Usiongeze viazi vibichi juu ya vile ambavyo vimeanza kukauka kwenye kaushio.
  • Acha viazi vipoe baada ya kuvitoa katika kaushio kabla ya kufungasha.

Vifaa

  • Kaushio bora
  • Kisu kikali kisichoshika kutu
  • Mabeseni

Malighafi

  • Viazi vitamu
  • Maji

Jinsi ya kukausha

  • Chagua viazi vilivyo bora
  • Osha viazi kwa maji safi na salama
  • Menya kwa kutumia kisu kikali kisichoshika kutu
  • Katakata ili kupata vipande vyenye unene upatao sentimita 6
  • Tumbukiza vipande kwenye maji yanayochemka. Chemsha kwa muda wa dakika 3 hadi 5 ili kuzuia shughuli za vimeng’enyo zinazoweza kubadili rangi ya viazi (browning).
  • Ipua na acha vipoe
  • Anika kwenye kaushio bora kwa kutandaza vizuri ilil kila kipande kipate jua sawa.
  • Viazi hivi hukauka kwa saa 6 hadi 7 kutegemea nguvu ya jua.
  • Kausha viazi hadi vifikie asilimia 9 ya unyevu na acha vipoe
  • Fungasha kwenye mifuko ya plastiki
  • Hifadhi sehemu baridi na kavu.

Viazi hivi huweza kuhifadhika kwa muda wa mwaka mmoja au zaidi bila kuharibika.

Matumizi

  • Hukaangwa au kuchemshwa na kuliwa.
  • Huchanganywa na vyakula vya mikunde kupata futari
  • Husagwa unga.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *