Mifugo

- Mifugo

Unafanya nini msimu huu wa mvua

Unakumbuka vile ng’ombe walivyokufa msimu wa ukame/kiangazi. Ulijiuliza ni kutokana na nini na je, msimu huu wa mvua unakusaidia vipi kujikinga na athari za kiangazi kwa msimu ujao. Hakikisha unafanya uzalishaji wa malisho kwa wingi msimu huu wa mvua kwa ajili ya kujikinga na athari za ukame. Je, umefikiia kuhusu malisho ya mifugo au umefikiria kuhusu kupunguza idadi ya mifugo.…

Soma Zaidi

- Mifugo

Ubora wa maziwa unatokana na usafi na utunzaji

Maziwa ni sehemu ya mlo kamili wenye virutubisho vya kutosha au viini lishe sawia vinavyohitajika katika mwili wa binadamu. Katika toleo lililopita, tulizungumzia kwa ufupi sana kuhusu usafi wa maziwa na mada hii tutaikamilisha kwa kueleza kwa undani vipengele kadhaa vinavyohusiana na usafi wa maziwa. Maziwa ni nini Maziwa ni maji meupe yenye viini lishe yanayokamuliwa kutoka kwenye mifugo mbalimbali…

Soma Zaidi

- Kuku, Mifugo

Jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe

Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa. Chakula cha kuku ni lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko ufuatao: Vyakula vya kujenga mwili kama vile…

Soma Zaidi

- Mifugo, Samaki

Uliza kuhusu samaki kama una changamoto unayopitia kwenye mradi wako

Kanyalo anauliza:Naomba kujua ni wakati gani ninatakiwa kubadili maji katika bwawa ikiwa maji ninayotumia ni ya kujaza? Muda wa kubalisha maji kwa kawaida siwezi kusema moja kwa moja ni baada ya muda kadhaa ila naomba unielewe kuwa uchafukaji wa maji katika bwawa inategemea na utunzaji katika bwawa lako. Mfano; ukilishia vyakula ambavyo sio sahihi kwa samaki huenda ukalazimika ukabadilisha maji…

Soma Zaidi

- Mifugo

Namna ya kutunza mifugo wakati wa msimu wa mvua

Ni ukweli usiopingika kwamba msimu wa mvua ni mzuri kwa ustawi wa mifugo. Hii ni kutokana na ongezeko la malisho kwa mifugo hasa kwa wafugaji wanaojishughulisha na ufugaji wa mifugo kama vile ng’ombe, kuku, sungura, mbuzi, kondoo, nguruwe, punda n.k. Msimu wa mvua kwa wafugaji huambatana na changamoto zisizo rafiki kwa maisha ya mifugo. Hii ni pamoja na magonjwa na…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Uvunaji wa maji ya mvua kuhakikisha usalama wa chakula

Ni vema kutumia fursa mbalimbali kuhakikisha usalama wa chakula. Katika miaka ya hivi karibuni hali ya hewa imekua ikibadilika mara kwa mara na kusababisha taharuki kwa watu wengi hasa wakulima. Mwezi wa kumi mwaka 2021, Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) ilitoa tahadhari juu ya kiwango cha mvua kati ya mwezi Novemba 2022 had Aprili 2022. Taarifa hio ilieleza mvua…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Kilimohai kimenifungua macho na kunionyesha fursa za kilimo

“Mwanzoni ni kama nilikuwa gizani, sikuwa najishughulisha na kitu chochote Zaidi ya kukaa nyumbani, sikuwahi kujua kama nina nguvu na nikisimama kama mama bora naweza kuzalisha vitu mbalimbali kwa faida ya familia yangu, hakika mimi ni kipofu niliyeona”. Ndivyo alivyoanza kueleza Bi. Renalda Lawrent, kutoka Kijiji cha Kambi ya simba (wilayani Karatu) ambaye kwasasa anajishughulisha na uzalishaji wa mazao mbalimbali…

Soma Zaidi

- Mifugo

Je, unafahamu kwa nini asali huganda?

Asali ni moja ya mazao yanayotokana na nyuki wakubwa au wadogo ikiwa katika kimiminika na yenye ladha ya sukari. Nyuki hutengeneza asali hii kwenye mzinga kwa kuchukua malighafi toka kwenye maua au miti yam aua ya aina mbalimbali na yanayopatikana katika eneo lilipowekwa mizinga. Asali hii huwa katika mfumo wa kimiminika yaani maji maji lakini wakati mwingine huweza kuganda bila…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo, Mimea, Redio, Shuhuda, Usindikaji

HERI YA MWAKA MPYA WA 2022

Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…

Soma Zaidi