Ngozi hukaushwa ili kuzuia uharibifu unaotokana na kuoza kwa kuwa si ngozi zote zinazozalishwa hupelekwa kiwandani zikiwa mbichi ili kusindikwa. Ngozi zikioza hupoteza ubora wake na hivyo kutokuwa na manufaa katika matumizi mbalimbali. Ngozi ni zao la mifugo linaloweza kutoa mchango mkubwa kuwainua kiuchumi wafugaji na jamii kwa ujumla. Baadhi ya wajasiriamali hutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na ngozi ya ng’ombe,…
Kilimo
Jifunze kusindika nazi na kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali
Kusindika nazi Katika msimu huu, nazi zinapatikana kwa wingi mashambani na sokoni na hivyo kufanya gaharama za uuzaji kuwa chini kidogo. Hata hivyo pamoja na upatikanaji huu, wakulima na wauzaji wengi hawajafikiria namna ya kuongezea thamani zao hili ili kuzalisha bidhaa bora zaidi zenye soko na muda mrefu wa matumizi. Mkulima Mbunifi unashauri kusindika nazi na kuzalisha bidhaa hizo ili…
Wasemavyo wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu
Mkulima Mbunifu imekua ikitembelea wakulima mbali mbali nchini Tanzania ili kuchukua shuhuda mbalimbali za wanufaika na kuzichapisha ziwe chachu kwa wasomaji wengine kujifunza na kufanya kwa vitendo. Je wewe umejifunza nini kutoka Mkulima Mbunifu? Tafadhali tuandikie kupitia mawasiliano yaliyo katika jarida hili. Katherini Samweli Palanjo, Kijiji cha Sura-Meru, Arusha Mimi ni mkulima wa kilimo hai, ninajishughulisha na kilimo cha mboga…
Unaweza kuongezea thamani Mtama kwa kuzalisha mvinyo
“Kwa karne nyingi, mtama umekuwa ukichukuliwa kama chakula cha watu maskini au chakula cha njaa, hili sasa limegeuka na kutoa matumaini mapya kwa wakulima wa mtama nchini Tanzania” Mtama ni kundi la mbegu ndogo ndogo aina ya mazao ya nafaka, yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe. Hii ni aina ya mazao yanayolimwa katika mazingira magumu kama…
Mahindi zao kuu la chakula linalopendwa na kutumiwa sana
Huu ni mwendelezo wa makala inayokuhusu kilimo cha mahindi kutoka toleo lililopita Inapendekezwa kuweka mbolea baada ya udongo kupimwa. Mbegu ya mahindi iliyoboreshwa inaweza kufanya vizuri inapowekewa mbolea halisi inayohitajika, kulingana na uhitaji wa virutubisho. Mbolea ya mboji inaweza kuwekwa kwenye shimo wakati wa kupanda. Palizi Hakikisha kuwa, shamba lako halina magugu ambayo hushindana na mazao kupata maji na virutubisho.…
Ujue mmea wa mnazi pamoja na kanuni za kilimo bora cha zao hili
Minazi ni zao la biashara nchini Tanzania ambalo hulimwa na kustawi zaidi ukanda wa pwani ya Tanzania. Mikoa kama Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba, pia kwa uchache Minazi hulimwa kwenye mikoa ya Mbeya, Kigoma na Tabora. Aina za minazi Kuna aina kuu tatu za Minazi inayolimwa hapa Tanzania nayo ni (i) Minazi…
Ijue teknolojia ya vijidudu vidogo vidogo na matumizi yake katika kilimo
Kumekuwa na changamoto kadhaa za kwenye kilimo ikiwemo kukosekana na rutuba magonjwa na wadudu waharibifu. Teknolojia ya EM imekuwa ikitumiwa nchi mbali mbali duniani na pia Tanzania. Baadhi ya maeneo ya ardhi hayana rutuba kutokana na mambo kadhaa kama vile kulimwa kwa muda mrefu au matumizi ya mbolea za viwandani. Ingawaje mbolea za viwandani zinasaidia kuongeza rutuba, lakini ni…
Fahamu aina mbalimbali za viungo muhimu kwa afya ya binadamu
Pamoja na viungo kutumika kuongeza ladha katika vyakula, pia vina manufaa katika mwili wa binadamu. Mara nyingi wakulima wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mazao muhimu kwa manufaa ya jamii, ilhali wao wakijisahau kuwa wanahitaji pia kutumia ili kuimarisha afya zao. Viungo mbalimbali kama tangawizi, vitunguu saumu, vitunguu maji, pilipili na limao ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili. Je ni…
Kwa nini tunafanya kilimo? Falsafa na umuhimu
Kilimo kimekuwepo tangu zama za mababu zetu. Binadamu wa kwanza walipata chakula chao kwenye mazingira yanayowazunguka na kwa juhudi kama uwindaji kabla ya kuanza kulima ardhi, kupanda mazao na kufuga mifugo kama vyanzo vya lishe. Hii ni pamoja na nafaka, mazao ya mizizi, karanga, matunda, nyama, maziwa, na hata mayai. Kilimo kimebadilisha maisha na maisha pia yamebadilisha muundo wa kilimo.…
Wakulima wanasemaje kuhusu masoko ya mazao ya kilimo hai
Mkulima anaezalisha kwa mazao kwa kufuata misingi ya kilimo hai, Bw. Zadock Kitomari alisema kuwa, unapoanza kujishughulisha na kilimo hai ambacho hakitumii kemikali unaona kuwa uzalishaji unakuwa mdogo lakini kwa kadri unavyoendelea uzalishaji unakuwa mkubwa. Anaeleza kuwa, kilimo hai ni aina ya kilimo kinachoangalia uhai wa mazingira, uhakika na usalama wa mlaji na usalama wa chakula jambo ambalo linamuhakikishia mkulima…