- Kilimo

Amrut Jal! kioevu cha udongo na kirutubisho cha kikaboni

Sambaza chapisho hili

Kama ilivyo kwa mwili wa binadamu unahitaji chakula chenye virutubisho, vivyo hivyo udongo wa kikaboni pia unahitaji kurutubishwa ili uweze kuzalisha vizuri.

Amrut Jal ni mbolea ya kioevu cha kikaboni ambacho huimarisha kiwango cha virutubisho katika udongo unaotumika kwa kilimo hai. Mkulima hana budi kujifunza namna ya kutengeneza na kutumia Amrut Jal katika shamba la kilimo hai.

Jinsi ya kutengeneza

Mahitaji

  • Mkojo wa ng’ombe
  • Kinyesi hai cha ng’ombe
  • Sukari guru nyeusi
  • Maji

Angalizo: Ikiwa sukari guru nyeusi haipatikani unaweza kutumia mbadala kama ndizi 6 zilioiva au tunda la fenesi lililoiva au glasi mbili za juisi ya muwa.

Jinsi ya kufanya

  • Changanya pamoja lita kumi (10) za maji, lita moja (1) ya mkojo wa ng’ombe, kilo moja (1) ya kinye­si freshi (hai) cha ngombe na kilo hamsini (50) ya sukari guru nyeusi.
  • Weka mchanganyiko huu kwa muda wa siku tatu (3).
  • Koroga mchanganyiko huu mara mbili au tatu kwa siku. (Koroga kwa kuzungusha upande wa kulia na tena kurudia upande wa kushoto)
  • Siku ya nne mchanganyiko huu utakua tayari.
  • Changanya sehemu moja ya mchanganyiko huu na sehemu ya kumi ya maji na Amrut jal itakua tayari kwa matumizi.

Jinsi ya kutumia

Chukua amrut jal uliotengeneza hapo juu, na ongeza kwenye udongo ambao umeandaa kufanya kilimo hai kila baada ya siku kumi na tano (15). Unaweza kuongeza majivu kwenye udongo kiasi cha kiganja cha mkono kwa matokeo bora zaidi.

Unaweza kuona kufanya kilimo hai inaweza kukugharimu kiasi kidogo cha pesa katika siku za mwanzo, lakini kadri unavyoendelea unabadilisha kulingana na mahitaji. Hivyo kilimo hai sio kigumu kutekeleza kama inavyofikiriwa

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *