Kilimo

- Kilimo, Mazingira, Udongo

Tumia majivu shambani

Majivu yana kiwango cha wastani wa madini kwa mgawanyiko tofauti, potasiamu 5% – 7%, kalishamu 25% – 50%, fosiforasi 1.5% – 2% na madini mengine kwa kiasi kidogo. Pia mabaki ya chenga za mkaa kwenye majivu yanasaidia kunyonya baadhi ya sumu kwenye ardhi. Matumizi Tumia kiasi cha kilo 2.5 mpaka 5 kitumike kwenye eneo la mita za mraba 33 au…

Soma Zaidi

- Kilimo

Fanya Kilimo mseto kwa uhakika wa chakula na utunzaji wa mazingira

Kilimo mseto ni njia ya kitamaduni, ambayo imekuwa ikitumiwa na wakulima barani Afrika na kwingineko tangu karne na karne. Njia hii hutoa fursa kwa wakulima kuweza kuzalisha mazao mengi na ya aina tofauti katika sehemu ndogo ya ardhi. Hii ni kwa sababu mazao hayo hupandwa kwa pamoja katika eneo hilo. Mbali na uzalishaji wa aina tofauti ya mazao, pia kilimo…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo

Namna rahisi kwa mkulima kulima zao la uyoga

Kabla ya kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa Uyoga. Mkulima wa kawaida anaweza kutumia kasha kama sehemu ya giza. Hatua muhimu katika kuotesha Uyoga Mkulima anatakiwa kwanza kutafuta mbegu, na baada ya…

Soma Zaidi

- Kilimo

Jarida la Mkulima Mbunifu ni darasa tosha la kilimo hai

“Mimi nilipata jarida la Mkulima Mbunifu mwaka 2017 Disemba kwenye maonyesho ya wakulima lakini mara baada ya kufika nyumbani sikulisoma nikaliweka kabatini wala sikufikiri kama linaweza kunisaidia kwa lolote, nilipokea kama kipeperushi tu”. Hayo ni maneno ya Bi. Magreth Leandry kutoka Kijiji cha Slahamo ambaye ni mfugaji lakini pia mkulima wa mazao mbalimbali kwa misingi ya kilimo hai. Bi. Magreth…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Uvunaji wa maji ya mvua kuhakikisha usalama wa chakula

Ni vema kutumia fursa mbalimbali kuhakikisha usalama wa chakula. Katika miaka ya hivi karibuni hali ya hewa imekua ikibadilika mara kwa mara na kusababisha taharuki kwa watu wengi hasa wakulima. Mwezi wa kumi mwaka 2021, Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) ilitoa tahadhari juu ya kiwango cha mvua kati ya mwezi Novemba 2022 had Aprili 2022. Taarifa hio ilieleza mvua…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Kilimohai kimenifungua macho na kunionyesha fursa za kilimo

“Mwanzoni ni kama nilikuwa gizani, sikuwa najishughulisha na kitu chochote Zaidi ya kukaa nyumbani, sikuwahi kujua kama nina nguvu na nikisimama kama mama bora naweza kuzalisha vitu mbalimbali kwa faida ya familia yangu, hakika mimi ni kipofu niliyeona”. Ndivyo alivyoanza kueleza Bi. Renalda Lawrent, kutoka Kijiji cha Kambi ya simba (wilayani Karatu) ambaye kwasasa anajishughulisha na uzalishaji wa mazao mbalimbali…

Soma Zaidi

- Kilimo, Udongo

Mbolea ya popo huongeza tija katika kilimo hai na kulinda rutuba ya udongo

Ni ukweli usiopingika kuwa, wakulima wengi kwasasa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mbolea kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali jambo ambalo huweza kutatuliwa kwa kutumia njia mbalimbali na matumizi sahihi ya mbolea za asili ikiwemo samadi itokanayo na kinyesi cha popo. Popo hupatikana katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye mapagala, miti, mapango au kwa kujenga…

Soma Zaidi

- Kilimo

Je, unafahamu kuwa kilimo hai kina kanuni zake za msingi

Kanuni za kilimohai zinavyofungamana na mazingira Kanuni ndio msingi wa kilimo hai na mchango unaoweza kuifanya dunia kuboresha kilimo duniani kwa ujumla. Kilimo ni moja ya shughuli muhimu zinazofanywa na binadamu kwa ajili ya kupata mahitaji ya kila siku ili kujikimu. Historia, mila na tamaduni za watu katika jamii zinaambatana na maendeleo katika kilimo. Kanuni zinazotumika katika kilimo kwa ujumla…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo, Mimea, Redio, Shuhuda, Usindikaji

HERI YA MWAKA MPYA WA 2022

Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…

Soma Zaidi