Sasa unaweza kushirikiana na jarida la MkM kutoa mafunzo na habari kwa wakulima kuhusu mbinu na teknolojia tofauti zinazowezesha kuboresha uzalishaji na kuleta faida kwa mkulima na jamii kwa ujumla. Hii ni fursa ya kuwekeza zaidi katika kufikisha matokeo ya utafiti na ubunifu unaowanufaisha wakulima kwa wakulima wenyewe. Kuna tafiti nyingi tu lakini njia za kusambaza kwa wakulima ni chache…
Kilimo
Kilimo hai hupambana na mabadiliko ya tabianchi
Mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia msingi wa maliasili katika sehemu kubwa ya ulimwengu hasa nchi zinazoendelea. Mabadiliko ya hali ya hewa huharakisha uharibifu wa mifumo ikolojia na kufanya kilimo kuwa kigumu kwa wakulima mashamba wenye madogo. Matokeo yake ni kwamba wakulima ambao ni muhimu sana kwa usalama wa chakula na uchumi wa mashinani wanakabiliwa na hali mbaya ya hewa…
Kujifunza kwa ushirikiano ni mbinu mbadala ya elimu ya kilimo
Katika mazungumzo na vikundi vya wakulima, mmoja wa wakulima walioshiriki katika mkutano wa kubadilishana mawazo kuhusu kilimo hai kama mbinu moja ya kilimo endelevu utafiti, alisema; “Kilimo hakilipi bili tena, na unajua haiwi rahisi.” Kauli hii ya mkulima huyu inaibua haja ya kufanya kilimo kuwa na maana kwa wakulima. Kwamba wanapofanya kazi wanachuma kutokana na jasho lao, yaani, jinsi ya…
Unaanzaje kilimo hai
Kumekua na maswali kadhaa juu ya kuanzisha kilimo hai. Yamkini, ewe pia unajiuliza swali hili, vile unavyoweza kuzalisha kwa mfumo wa kilimo hai shambani mwako. Jarida la Mkulima Mbunifu ni mahususi kwa ajili yako na katika makala hii tunakukumbusha tena. Kama una nia thabiti ya kuanzisha kilimo hai, fuata hatua zifuatazo; Angalia uwezekano wa kupata soko kwanza Jiulize mwenyewe: Ni…
Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao ambayo yanapandwa ili kuongeza rutuba kwenye udongo
Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na: Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo. Zinaongeza tani nyingi za viumbe hai kwenye udongo, hivyo basi, kuongeza udongo wenye rutuba, uwezo wa kutunza maji,…
WEBSITE DESIGNER
Terms of Reference: Updating Mkulima Mbunifu Website – www.mkulimambunifu.org About Mkulima Mbunifu (MkM) Mkulima Mbunifu (MkM) Magazine is a Farmer Communication Programme project that is implemented in Tanzania since July 2011 with support from Biovision Foundation, Switzerland and Biovision Africa Trust (BvAT), Nairobi, Kenya. The publication aims to provide information to smallholder farmers to enable them adopt improved sustainable agriculture…
Ni muhimu kuzingatia soko la mazao kabla ya uzalishaji
Suala la soko ni la msingi na ni la wakati wote, kuanzia kipindi cha utafutaji taarifa ya zao husika, wakati zao likiwa katika hatua ya awali ya uzalishaji na hata linapokuwa tayari kwenda sokoni. Ni muhimu kwa mkulima kutafuta soko la mazao yake ili aweze kuuza kwa bei iliyopo sokoni na ikiwa bei imeshuka kwa ghalfa bila kutarajiwa, aweze kufikiri…
Umuhimu wa udongo kwa uzalishaji wenye tija
Udongo wenye afya ni udongo ulio hai, ambao unazalisha mazao bora na yenye afya. Udongo lazima uwe na minyoo na viumbe vingine. Viumbe hawa hufanya kazi ya kulainisha udongo kwa kuvunjavunja masalia ya majani, mimea na mabua yaliyokufa kisha kubeba masalia hayo hadi chini ya udongo na kuichanganya kisha kuzalisha virutubishi vya kwenye mimea. Viumbe hawa huongeza kasi ya kuoza…
Kilimo bustani huongeza pato nyumbani
Kilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo. Kilimo cha bustani ni chanzo cha ajira na pato kwa wakulima na watu wengine. Mboga na matunda vinatupatia virutubisho vya kujenga, kutia nguvu na kulinda mwili. Unapowaangalia wakulima utagundua wengi wamejikita katika uzalishaji wa mazao ya bustani, kwa lengo la kukidhi mahitaji…
Matokeo ya lishe duni kwa watoto na jinsi ya kuboresha afya
Kila mwaka, watoto wengi chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufa kwa sababu ya lishe duni na chakula. Watoto hawa hawapati chakula chenye vitamini, madini ya iodini na chuma ambayo yanahitajika kwa afya na ukuaji mzuri. Hali hii inasababisha utapiamlo. Watoto wenye umri wa miezi 6 na zaidi, wapewe chakula cha ziada tofauti-tofauti kwa viwango vidogo mwanzoni na kuongeza kadri…








