Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika kilimo na mbinu za uzalishaji. Utafiti umeonyesha kuwa mbinu asilia za kilimo hai zina faida zaidi kuliko zile zinazojumuisha kemikali au vitu vingine hatari. Siku hizi, bidhaa za kilimo hai zinapatikana kwa urahisi katika maeneo mengi. Hii inamaanisha kuwa kuna ushindani kati ya wazalishaji wa kilimo hai. Ikiwa unataka kufanikiwa…
Kilimo
Mkulima hupaswi kuwa maskini
Swali hili limekuwa likijirudia mara kwa mara, kuwa ni kwa nini wakulima wawe maskini? Kwa watu walio wengi hata wakulima wenyewe, wana majibu mengi sana ambayo wamekuwa wakiyatoa, hasa katika kutetea huko hiyo, huku wakiweka kuwa wao ni watu wa chini na wanaokubaliana na hali hiyo ya umaskini. Kuna wale ambao watasema kuwa ni maskini kwa sababu ya zana duni…
Ifahamu ndizi kitarasa na faida zake
Ndizi ya Kitarasa ni moja ya ndizi inayotumika kama chakula cha kitamaduni kwa wachaga waishio katika mkoa wa Kilimanjaro. Aina hii ya ndizi hutumiwa kutengeneza unga wa uji, kutengeneza bia ya kitamaduni na kama mchanganyiko wa chakula cha kitamaduni katika sahani. Hata hivyo, wazalishaji wa kitarasa walipungua, kutokana na mabadiliko ya utamaduni, mtindo wa maisha, upatikanaji duni wa soko na…
Tengeneza mbolea ya chai ya alizeti pori (Tithonia diversifolia)
Alizeti pori maarufu kisayansi tithionia diversifolia ni aina ya mmea unaomea karibu kila mahali kando ya barabara na hata kwenye kingo za mito katika ardhi isiyokuwa na rutuba au hata katika maeneo ya bustani. Mmea huu ni mrefu na una mashina mengi kuanbzia sehemu ya chini hadi sehemu kunakotoa maua. Kwenye udongo wenye rutuba, mmea huu huweza kufikia urefu wa…
Maharagwe ya ngwara: Muunganiko wa lishe ya kiafrika
Ngwara ambalo pia hujulikana kama Fiwi, ni aina ya maharagwe katika familia ya Fabaceae. Asili yake ni katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na hulimwa katika maeneo ya kitropiki. Zao hili lenye utajiri wa virutubisho, ambalo kwa muda mrefu lilisahaulika, sasa limeanza kupata umuhimu mkubwa kutoka kwa wadau wa kilimo. Zao hili linastawi katika hali ya hewa…
Je, njia za asili za kukabili wadudu na magonjwa ni zipi?
Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara wanayoleta kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakua na uwiano basi sehemu moja inaweza kuwa na idadi kubwa ya wadudu waharibifu hivyo kusababisha madhara. Madhumuni ya njia hizi za asili ni kujaribu kuweka uwiano katika mazingira. Mfumo huu haukusudii kuangamiza wadudu bali kuwakabili. Ni bora basi kuchukua tahadhari na kuzuia…
Pitaya, tunda jipya linaloweza kulimwa sehemu kame
Kwa Tanzania matunda ya dragon au kama yajulikanavyo kwa kiswahili Pitaya au Pitahaya ni aina mpya. Matunda haya asili yake ni Mexico au maeneo ya Amerika Kaskazini lakini kwa sasa yanalimwa sana bara la Asia na kwa ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa yanalimwa Kenya. Kwa sababu ya kutolimwa sana Tanzania, matunda yake ni aghari huuzwa kati ya Sh 10,000/…
Je, wajua sababu kumi za kuendeleza kilimo hai
Chakula kinakuwa na ladha ya asili: ladha yake ni nzuri Kimesheheni viinilishe vya asili vya kutosha kwa afya: kwa asili kinajenga afya. Hakina mabaki hatarishi ya kemikali: hakina kemikali Kinaepusha matumizi ya vyakula vilivyobadilishwa vinasaba /GMO: kinatunza afya ya mlaji Havisababishi magonjwa yanayosababishwa na upulizaji wa kemikali kwa mkulima wala mlaji: mkulima na mtumiaji/ mlaji hubakia salama Kinahimiza utunzaji wa…








