- Kilimo, Mimea, Udongo

Unaanzaje kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Kumekua na maswali kadhaa juu ya kuanzisha kilimo hai. Yamkini, ewe pia unajiuliza swali hili, vile unavyoweza kuzalisha kwa mfumo wa kilimo hai shambani mwako. Jarida la Mkulima Mbunifu ni mahususi kwa ajili yako na katika makala hii tunakukumbusha tena.

Kama una nia thabiti ya kuanzisha kilimo hai, fuata hatua zifuatazo; Angalia uwezekano wa kupata soko kwanza

Jiulize mwenyewe:

  • Ni wapi na kwa nani naweza kuuza mazao yangu?
  • Naweza kuuza kwa bei gani?
  • Ni kiasi gani naweza kuzalisha ili kuwapatia wateja wangu?
  • Ni nani washindani wangu?
  • Kuna mkulima yeyote au kikundi cha wakulima ambacho kimefanikiwa katika kilimo hai, na je naweza kuungana nao, au naweza kujifunza kutoka kwao?

Kwa ufupi, unapozalisha bidhaa kwa soko lolote, hatua ya kwanza wakati wote ni kutambua soko na wanunuzi. Ni lazima iwe wazi kuwa ni wapi pa kuuza na ni nani utamuuzia kabla ya kuanza kuzalisha!

Vigezo vingine unavyopaswa kuzingatia vinajumuisha: umbali wa sokoni, bei sokoni, gharama za uzalishaji wa bidhaa yako, na muda bidhaa zako zinaweza kukaa (kipindi gani unaweza kuuza bidhaa zako kabla ya kuanza kuharibika).

Majaribio ya uzalishaji wa kilimo hai

Ukishakuwa na uhakika kuwa utauza mazao utakayozalisha kwa misingi ya kilimo hai, jaribu kwanza katika eneo ndogo ili kuepuka hatari ya kupoteza mavuno ya awali. Pia, unaweza kuangalia namna ya kutengeneza bidhaa nyingine kutokana na mazao hayo, kama kutengeneza jamu na bidhaa zingine za thamani ya juu.

Panua uzalishaji

Tekeleza hili pale tu unapoona kuwa inafaa na utauza bidhaa zako kwa faida. Ili kuzalisha zaidi, ongeza eneo na uwajumuhishe wakulima wengine.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *