Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…
Kilimo Biashara
Utengenezaji wa jibini ngumu
Hii ni jibini aina ya cheddar ambayo asili yake ni huko Uingereza lakini kwasasa hutengenezwa katika nchi mbalimbali dunian. Hatua za utengenezaji Pima ubora wa maziwa Pasha moto maziwa kufikia nyuzi joto 65C yaache katika joto kwa dakika 30 au nyuzi joto 71.5C kwa sekunde 15 Poza maziwa kufikia nyuzi joto 22 hadi 25C Weka kimea cha mtindi (mesophilic) asilimia…
EMAS: Kirutubishi chenye matumizi mengi kwa mkulima
Mlima bora ni yule anayetumia malighafi sahihi ili kuzalisha mazao mengi yenye tija na salama kwa chakula. EMAS ni nini? EMAS Effective Micro Organisms Active Solution ni namna nyepesi ya kutengeneza bakteria wazuri ama rafiki kwa njia ya kimiminika ambacho ni rahisi kutumia na pia ni salama. Mahitaji Maziwa Fresh lita 10 Maji ya mchele lita moja Molasesi lita 10…
Uzalishaji wa malisho
Bonyeza hapa na sikiliza kuhusu malisho aina ya matete na faida zake
TUNAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KUTUMA JARIDA LA OKTOBA
Habari ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu. Ni matumaini yetu kuwa uko salama na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukutumia nakala yako ya jarida la Mkulima Mbunifu. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto kidogo zilizokuwa nje ya uwezo wetu ambazo zimepelekea kusindwa kuchapisha nakala ya mwezi Oktoba kwa wakati. Jarida hili…
Tunaomba radhi kwa kutokusikika hewani
Ndugu msikilizaji na mfuatiliaji wa vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu/SAT, tunaomba radhi kutokana na kipindi chetu kilichokusudiwa kurushwa hewasi siku ya jumamosi tarehe 30 Oktoba 2021 kutokusikika. Hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Sasa kipindi hicho cha kilimo kilichokuwa kinahusu kilimo mseto na kilimo cha mzunguko wa mazao kitarushwa upya siku ya jumamosi ya tarehe…
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…
Sindika machungwa kuepuka hasara na upotevu usio wa lazima
Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa sana kwa wingi katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Mwanza. Zao hili ni la chakula na biashara. Ikiwa huu ni msimu wa machungwa, wakulima hawana budi kujifunza namna mbalimbali za kusindika zao hili ili kuondokana na upotevu unaotokana na wingi wake na kukosekana kwa soko…
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…