Habari ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu. Ni matumaini yetu kuwa uko salama na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukutumia nakala yako ya jarida la Mkulima Mbunifu. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto kidogo zilizokuwa nje ya uwezo wetu ambazo zimepelekea kusindwa kuchapisha nakala ya mwezi Oktoba kwa wakati. Jarida hili…
Shuhuda
Tunaomba radhi kwa kutokusikika hewani
Ndugu msikilizaji na mfuatiliaji wa vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu/SAT, tunaomba radhi kutokana na kipindi chetu kilichokusudiwa kurushwa hewasi siku ya jumamosi tarehe 30 Oktoba 2021 kutokusikika. Hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Sasa kipindi hicho cha kilimo kilichokuwa kinahusu kilimo mseto na kilimo cha mzunguko wa mazao kitarushwa upya siku ya jumamosi ya tarehe…
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…
Mama shujaa wa chakula (Elinuru Palangyo)
Nafurahia kua mnufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu. Jarida hili limenifunza mambo mengi. Mimi kama mkulima wa kilimo hai, mbinu za kilimo hai nimejifunza kupitia jarida la Mkulima Mbunifu. Mbali na kupata elimu ya kilimo hai nimefahamika na watu wengi, mmoja mmoja na pia mashirika binafsi naya kiserikali. Kwani, nimekua nikishiriki nane nane na sasa nina shamba darasa ambalo ninatumia…
Miaka 10 ya Mkulima Mbunifu na kilimo hai
Mkulima Mbunifu imechangia kwa asilimia kubwa kufahamika na kutekelezwa kwa kilimo hai nchini Tanzania. Hii ilikuwa ni ndoto ambayo imegeuka na kuwa kweli. Watanzania wengi na baadhi ya wakulima wa nchi jirani wameelimika na kufahamu kwa kina kuhusu kilimo endelevu kupitia MkM. Ninafuraha kubwa kushiriki katika kuifanya ndoto hii kutimia na kuendelea kuwa msaada kwa uwepo wake. Wazo la uwepo…
Mkulima Mbunifu imeniongezea uwezo katika uzalishaji
Nilianza kupokea jarida la Mkulima Mbunifu toka mwaka 2012 (Miaka 9 sasa) na kupitia jarida hili nimeweza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu kilimo pamoja na ufugaji (Rubia Issa- Kondoa, Dodoma) Mimi ni mkulima wa alizeti, mahindi na maharage lakini kupitia MkM nimeweza kujifunza kuhusu uchavushaji wa mazao kwa kutumia nyuki hasa alizeti hivyo nikaamua kuwa mfugaji wa nyuki. Kwa mradi huu…
Mkulima Mbunifu limenifaidisha sana kupitia uzalishaji wa kilimo hai
Nilianza kupokea majarida ya Mkulima Mbunifu kwa zaidi ya miaka 5 sasa (Eliakarimu G. Gayewi wa kikundi cha Dilega Katesh mkoani Manyara). Nashukuru sana kuwa sehemu ya wanufaika wa jarida hili kwani toka nianze kupokea nimejifunza na kufaidika na mambo mengi kwenye kilimo na ufugaji. Kuna elimu nyingi kuhusu kilimo zinazotolewa kwenye jarida hili ambayo sikuwa najua kwani nilikuwa nalima…