- Shuhuda

Mama shujaa wa chakula (Elinuru Palangyo)

Sambaza chapisho hili

Nafurahia kua mnufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu. Jarida hili limenifunza mambo mengi. Mimi kama mkulima wa kilimo hai, mbinu za kilimo hai nimejifunza kupitia jarida la Mkulima Mbunifu.

Mbali na kupata elimu ya kilimo hai nimefahamika na watu wengi, mmoja mmoja na pia mashirika binafsi naya kiserikali. Kwani, nimekua nikishiriki nane nane na sasa nina shamba darasa ambalo ninatumia kufundisha watu wanaohitaji elimu ya kilimo hai.

Kwakweli kama hujajisajili kupokea jarida hili unakosa mambo mengi sana ya muhimu kupitia jarida hili. Watafute Mkulima Mbunifu wanapatikana na ushauri utapata kwa wataalamu wanao shirikiana nao.

Ninawapongeza Mkulima Mbunifu kwa kufikia miaka kumi mkituelimisha sisi wakulima wadogo. Tunaomba msiache na zaidi mpanue wigo wa kufikia watu wengi, kwani ninaamini wahitaji wa jarida hili ni wengi na hawajapata fursa kuliona.

Ninawaombea wafadhili waendelee kuwawezesha ili muendelee kutuhabarisha. nawapongeza pia kwa jitihadada za vipindi vya radio ambavyo mmekua mkirusha mara moja moja.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *