Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Mimea
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea
Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu. Hii ni hali ya kimaumbile katika kusawazisha idadi. Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuzidi idadi na kusababisha madhara. Madhumuni ya njia ya kiasili…
Fahamu namna ya kuandaa na kupanda mbegu za maembe
Wakulima walio wengi nchini Tanzania, wamekuwa wakipanda aina mbalimbali za miti ya matunda, bila kuzingatia kanuni na taratibu za upandaji wa miti hiyo, jambo ambalo limekuwa likiwasababishia hasara kwa kuwa na miti isiyokuwa na tija. Ni muhimu kwa wakulima wa miti ya maembe kufahamu na kuzingatia taratibu za uandaaji wa mbegu za kupanda katika eneo yako. Hili linaweza kufanyika kwa…
Ukizingatia kanuni sahihi, kilimo cha migomba kina tija
Nchini Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya. Zao la migomba limekuwa muhimu, na kufuatiwa na mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo, viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharagwe. Zao la…
Ijue teknolojia ya vijidudu vidogo vidogo na matumizi yake katika kilimo
Kumekuwa na changamoto kadhaa za kwenye kilimo ikiwemo kukosekana na rutuba magonjwa na wadudu waharibifu. Teknolojia ya EM imekuwa ikitumiwa nchi mbali mbali duniani na pia Tanzania. Baadhi ya maeneo ya ardhi hayana rutuba kutokana na mambo kadhaa kama vile kulimwa kwa muda mrefu au matumizi ya mbolea za viwandani. Ingawaje mbolea za viwandani zinasaidia kuongeza rutuba, lakini ni…
Fahamu aina mbalimbali za viungo muhimu kwa afya ya binadamu
Pamoja na viungo kutumika kuongeza ladha katika vyakula, pia vina manufaa katika mwili wa binadamu. Mara nyingi wakulima wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mazao muhimu kwa manufaa ya jamii, ilhali wao wakijisahau kuwa wanahitaji pia kutumia ili kuimarisha afya zao. Viungo mbalimbali kama tangawizi, vitunguu saumu, vitunguu maji, pilipili na limao ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili. Je ni…
Mchicha: Zao la muda mfupi lenye faida
Wakati wakulima wakijikita kwa kiasi kikubwa kwenye mazao mengi ya bustani kama vile nyanya, karoti,kabichi na mengine mengi, hawana budi pia kuweka mkazo katika zao la mchichi ambalo huvunwa kwa muda mfupi (wiki 3 – 5) na lenye pato kubwa katika masoko makubwa. Halikadhalika, mkulima hawezi kuwa na gharama kubwa kwenye kilimo cha mchicha hasa kwa kuwa ni zao la…
Jinsi ya kukausha uyoga na kuhifadhi kwa muda mrefu
Uyoga ni moja ya vyakula muhimu katika mwili wa binadamu, vinavyoupa mwili nguvu na virutubisho vya kujenga mwili. Uyoga ni mmea uliopo katika kundi la mimea aina ya fangasi, na umetajwa na wataalamu mbalimbali kuwa na faida kwenye suala la afya kwa binadamu ikiwa ni pamoja na kuondoa seli mfu zilizoko mwilini. Kilimo cha uyoga ni rahisi na unaweza ukavuna…
Tumia eneo ndogo kuanzisha bustani ya nyumbani
Bustani ya nyumbani ni eneo lililokaribu na nyumbani au jikoni ambalo linaweza kutumika kwa kulima aina mbalimbali za mboga, matunda na viungo vya chakula. Jinsi ya kuandaa bustani ya gunia Mahitaji muhimu Gunia au mfuko wa salfeti iliotobolewa pande zote Kokoto au mawe madogo Nguzo au ubao wa 4’ kwa 2’ wenye urefu wa mila moja na nusu Mbolea ya…