- Mimea

Fahamu namna ya kuandaa na kupanda mbegu za maembe

Sambaza chapisho hili

Wakulima walio wengi nchini Tanzania, wamekuwa wakipanda aina mbalimbali za miti ya matunda, bila kuzingatia kanuni na taratibu za upandaji wa miti hiyo, jambo ambalo limekuwa likiwasababishia hasara kwa kuwa na miti isiyokuwa na tija.

Ni muhimu kwa wakulima wa miti ya maembe kufahamu na kuzingatia taratibu za uandaaji wa mbegu za kupanda katika eneo yako.

Hili linaweza kufanyika kwa kushirikiana na wataalamu wa miti, au kupata taarifa sahihi kutoka katika vyanzo sahihi vyenye taarifa ambazo zimejumuisha wataalamu na watafiti.

Zifuatazazo ni njia za kuandaa na kupanda mbegu za embe;

  • Tumia matunda yaliyoiva vizuri na yenye maumbile halisi kwa ajili ya mbegu.
  • Ondoa nyama ya nje ya kokwa, ama kwa kula tunda au tumia njia nyingine.
  • Safisha kokwa ili kuondoa utelezi. Unaweza kuloweka kokwa kwenye maji kwa siku mbili au zaidi ili utelezi uondoke kwa urahisi zaidi.
  • Ondoa gamba la kokwa kwa kukata na mkasi wa kupogolea au kisu ili uipate mbegu ya ndani.

Kuondoa ganda la kokwa kuna faida zifuatazo;

  • (a)  Kunatoa nafasi ya kuona mbegu halisi kama ni nzima au imeharibika.
  • (b)  Mbegu iliyoondolewa ganda inaota mapema (siku 10-14) ukilinganisha na mbegu isiiyoondolewa ganda (itachukua siku 28 au zaidi).

Kuandaa tuta na kupanda mbegu za embe

  • Andaa tuta lenye kimo cha sentimeta 20 (mchoro 1).
  • Tumia udongo unaopitisha maji kwa urahisi (udongo wa kichanga au mchanga halisi ni bora zaidi).
  • Sawazisha vizuri sehemu ya juu ya tuta.
  • Kupanda mbegu za embe
    • Weka alama za mistari kwenye tuta kwa nafasi ya sentimita ishirini (20) kati ya mstari hadi msitari.
    • Panda mbegu kwa kuelekeza sehemu ya kiotea cha mzizi iwe chini na sehemu ya kiotea cha shina/tawi iwe
    • Tenga nafasi ya sentimita kumi (10) kutoka mbegu hadi mbegu katika msitari.
    • Fukia mbegu kwa udongo/mchanga kwa kima cha sentimeta moja (1).
Jinsi mbegu inavyochipua

Mwagilia maji kila yanapohitajika. 
Miche ya miembe iliyopandwa katika kitalu cha awali inahitaji kupandikizwa katika kitalu cha pili (viriba). Miche ya miembe huhamishiwa kwenye kitalu cha pili inapokuwa na majani halisi 2-4 yaliyokomaa.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *