Mimea

- Kilimo, Mimea

Tushirikiane kupata soko la mazao ya kilimo hai

Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai. Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwendo, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mimea

Usindikaji wa ndizi ili kuongeza kipato

Zao la migomba lina asili ya Philipino. Shina la mgomba limeundwa na vikonyo vya majani 12 hadi 30, kila kimoja kikiwa na urefu wa mita 7.6. Vikonyo hivyo pamoja na majani ya migomba hutumika kutengenezea nyuzi. Pamoja na nyuzi, zao kuu linalotokana na migomba ni ndizi, ambazo pamoja na kuwa ni chakula cha binadamu, lakini pia hutumika kwa njia nyinginezo…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo, Mimea

Gliricidia: Mti wenye faida lukuki kwa mkulima

Gliricidia ni mti ambao kisayansi hujulikana kwa jina la gliricidia sepium ambao hutumika kwa ajili ya mbolea au kurutubisha ardhi. Mti huu wa gliricidia ni  jamii ya miti ya malisho ambayo majani yake hutumika kurutubisha udongo na kulishia mifugo hasa katika kipindi cha ukame. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kumudu kuzalisha wakati wa kiangazi pamoja na kudumisha hali…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mimea

Samadi ya wanyama na mimea

Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni. Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho. Samadi iliyo tayari kwa matumizi Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mimea

Mapapai bora hupelekea soko lenye tija

Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamin A na madini ya kalsiamu kwa wingi na zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini kwa wastani wa tani 2,582 kwa mwaka. Ili kuweza kuzalisha zao la papai kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa ni muhimu kuhakikisha unazingatia kanuni zote za kilimo bora za uzalishaji wa mapapai. Ubora…

Soma Zaidi

- Mimea

Nimepiga hatua kwa kulima Canavalia

“Nilikuwa naotesha ekari tatu za mahindi na maharage lakini niliishia kuvuna chini ya gunia 10 za mahindi lakini pia nikipata maharage kidogo sana”. Hivyo ndivyo alivyoanza kueleza Bi. Edvester O. Yambazi (68), mkazi wa Sanya Juu ambaye kwasasa ameamua kufanya kilimo cha mahindi huku akiotesha zao funikizi aina ya Canavalia. Safari ya kilimo Bi. Yambazi anaeleza kuwa, aliteseka kwa muda…

Soma Zaidi

- Mimea

Namna bora ya kuvuna na kusindika mbaazi

Nimelima zao la mbaazi kwa muda mrefu sana, na miaka yote nimekuwa nikipata faida, mpaka hivi karibuni bei ya zao hili ilipoanguka na tukapata hasara. Je ni namna gani naweza kuhifadhi zao hili au kusindika? Msomaji MkM-Arusha. Mbaazi ni kati ya mazao jamii ya mikunde ambayo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mtwara, Dodoma, Lindi, Pwani, Morogoro, Arusha, Manyara, Tanga…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mazingira, Mimea

Rutuba ya udongo ndio uhai wa udongo na tija kwa mkulima

Ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha anauilisha udongo kwa kutumia virutubisho vya asili, ili kuweza kuwa na rutuba na kuzalisha mazao yenye tija. Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho. Vipengele…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mimea

Tumia mazao funikizi kwa chakula na kulisha mifugo

Mazao funikizi siyo mageni sana kwa wakulima walio wengi isipokuwa kwa wale ambao ndio kwanza wanaanza kujiingiza katika kilimo hifadhi. Si mazao yote funikizi yanayoweza kutumika kulishia mifugo moja kwa moja mara baada ya kuvuna kutoka shambani. Mengine ni lazima yafanyiwe maandalizi fulani ndipo yatumike kulishia. Mazao funikizi kama vile, canavalia yanahitajika kukaushwa kwanza na kuandaliwa vyema kabla ya kulisha…

Soma Zaidi