Kilimo cha Giligilani (Coriander) ni mradi mkubwa unaojitosheleza kukuza maisha ya mkulima kutokana na sababu kuwa zao hili la biashara huchukua muda mfupi toka kuotesha hadi kuvuna. Zao hili linalotumika kama kiungo cha chakula katika mapishi ya vyakula mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi linafaa kulimwa wakati wowote na katika maeneo mengi ya Tanzania hususani mikoa ya Mbeya na Iringa.…
Mifugo
Soko la mbogamboga hutokana na uzalishaji makini
Soko ni mahali au njia ambayo muuzaji na mnunuzi hukutana na kubadilishana mali au huduma. Ni fursa ya kuuaza na kununua. Kwa kawaida tunapozungumzia soko, tunagusia mambo kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na ukubwa wake, yaani wingi wa wauzaji na wanunuzi katika soko husika, ushindani, washindani, bidhaa na bei zake, changamoto, pamoja na mabadiliko yanayotegemewa. Kwa upande mwingine, tunaweza…
Fahamu wadudu wasumbufu katika ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku ni moja ya sekta ambayo imekuwa na faida kwa wafugaji walio wengi, na hata watu ambao wanafanya shughuli nyinginezo, lakini bado hujishughulisha na ufugaji wa kuku. Pamoja na aina hii ya ufugaji kuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea wafugaji kipato kikubwa, bado inakumbwa na changamoto mbalimbali. Mojawapo ya changamoto hizo ni pamoja na uwepo…
Ugonjwa wa ng’ombe wa mapele ngozi
Ugonjwa wa mepele ngozi, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kisayansi kwa jina la Capri poxvirus. Takribani asilimia 5 hadi 50 ya ng’ombe katika kundi wanaweza kupatwa na ugonjwa huu, ambapo ng’ombe wa umri wowote anaweza kupatwa na ugonjwa huu. Ugonjwa wa mapele ngozi hauambukizwi kwa binadamu. Chanzo cha maambukizi na namna ugonjwa unavyoenea Maji maji yanayotoka kwenye vidonda na…
Tuelimishane kuhusu mradi wa samaki kwa uzalishaji wenye tija
Ni mazingira gani yanafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki! Emma Peter anauliza: Nimefuatilia sana huu ujasiriamali kweli nimevutiwa na ningependa kujaribu kufanya. Nina eneo Rukwa lenye maji yakutosha ya asili takribani mita za mraba 2000, naomba ushauri wako Musa, Jinsi ya kuandaa hayo mabwawa na wapi nitapata samaki hasa sato maeneo ya Mbeya au karibu na Rukwa. Musa Said anajibu:…
Namna ya kuhifadhi mahindi kulinda ubora na kukidhi mahitaji ya chakula
Mahindi ni zao la kwanza katika mazao makuu ya nafaka hapa nchini. Huzalishwa kwa wastani wa tani 2393000 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 63 ya mazao yote ya nafaka nchini. Zao la mahindi hulimwa karibu katika mikoa yote, lakini hulimwa zaidi katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Mwanza na Shinyanga. Licha…
Karibu maonyesho ya Nane Nane 2020
Kama ilivyo ada kila mwaka nchini Tanzania, wakulima hujumuika pamoja kusherehekea wiki ya kitaifa ya kilimo ambayo hufanyika kikanda nchini Tanzania. Maonyesho hayo mahususi hutoa fursa kwa wakulima kufahamiana na kuonesha bunifu mbalimbali, nyenzo za kilimo, usindikaji na masoko ya bidhaa mbalimbali za kilimo. Mwaka huu maonyesho hayo yatafanyika kitaifa mkoani Simiyu, Mkulima Mbunifu itashiriki kikamilifu hivyo usiache kututembelea katika…
Fahamu na dhibiti ugonjwa wa Coenurosis
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na viluwiluwi vinavyojulikana kitaalamu kwa jina la Coenurusis Cerebralis unaoshambulia mfumo wa fahamu wa kati (ubongo na uti wa mgongo) wa mbuzi na kondoo. Chanzo cha viluwiluwi Viluwiluwi vya ugonjwa huu vinatokana na minyoo aina ya tiniamaltisepts iliyopo katika utumbo wa mbwa au wanyama pori jamii…
Zalisha bilinganya nyeupe kuongeza pato na lishe
Bilinganya nyeupe (Long White Eggplant) ni moja ya zao la mbogamboga ambalo lina viini lishe vingi na muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, Vitamini A, B na C, wanga, protini na maji. Kisayansi zao hili hujulikana kama Solanum Melongenai na kilimo chake huweza kufanyika katika majira yote ya mwaka. Hali ya Hewa Zao hili huhitaji hali ya…
Jifunze namna ya kuhifadhi mazao ya mikunde baada ya mavuno
Kabla mkulima hajavuna mazao yake, ni vyema akatambua namna ya kuyahifadhi kwa lengo la kuhakikisha zao linabaki katika ubora wake kwa muda mrefu. Kwa nini kuhifadhi Mazao yanapovunwa, ni vyema kuhifadhiwa ili kuhakikisha usalama wa chakula katika kaya na taifa kwa ujumla. Kuweka akiba kwa matumizi ya baadaye au kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya mbegu. Mikunde huhifadhiwa kwenye maghala…






