“Miongoni mwa mafanikio niliyoweza kupata kutoka katika makala mbalimbali za jarida la Mkulima Mbunifu ni pamoja na; ufugaji wa nyuki, uanzishaji wa vitaru vya miti, kilimo cha mboga mboga kwa kutumia mbolea ya asili, pia nimeweza kuboresha uzalishaji wa samaki kwa kutumia lishe ambapo imenisaidia kupata kitoweo. Kutokana na haya kipato changu kimeongezeka na kumudu majukumu ya familia. Hii ni…
Mifugo
Ufugaji wa ndani wa kuku wa asili na banda bora la kufugia
Katika toleo lililopita tulielezea kwa undani kuhusu ufugaji wa kuku wa asili pamoja na mifumo ya ufugaji ikiwa ni mfumo huria na nusu huria. Katika toleo hili tutaangazia mfumo wa ndani na banda la kuku. Mfumo wa ndani ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani huku wakipatiwa chakula na maji. Kuku kufanyiwa huduma nyingine muhimu wakiwa…
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na unamuda wa kuwahudumia wanyama hawa. Ufugaji wa sungura si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa. Sungura wanahitaji uangalizi hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu. Mabanda Kuna aina mbili ya mabanda ya kufugia: Kwanza ni mabanda ya kufugia ndani muda wote…
Njia zinazotumika kutibu udongo wa kusia mbegu katika viriba
Uoteshaji na usiaji wa mbegu katika viriba ni teknologia inayokua siku hadi siku. Zipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika katika kutibu udongo unaotumika kwenye viriba ili usiwe chanzo cha kusambaza vimelea vya magonjwa. Udongo Mchanganyiko wa udongo unaotumika katika viriba unatakiwa uwe na sifa zifuatazo; Uwe na rutuba ya kutosha. Usiwe wenye kutuamisha maji, lakini uweze kuhifadhi unyevu wa kutosha. Unaoruhusu…
Afya ya mifugo hutegemea uangalizi wa kina na tiba sahihi
Afya ya mifugo ni tatizo kubwa linalowakabili wafugaji walio wengi katika sehemu mbalimbali za nchi. Wapo wataalamu mbalimbali katika maeneo na mikoa yote ya nchi wanaotoa huduma ya mifugo lakini, bado kuna changamoto nyingi zinazowakumba wafugaji. Katika sehemu ambazo mawasiliano na miundo mbinu ni duni, wafugaji wamekuwa wakipoteza mifugo kutokana na sababu kuwa mara ugonjwa unapoikumba inakuwa si rahisi kufikiwa…
Chakula cha nguruwe kinahitaji virutubisho sahihi
Nguruwe huhitaji kulishwa vizuri ili waweze kukua haraka na kufikia uzito wa kuchinjwa mapema. Ikiwa watatunzwa vizuri watafikia uzito wa kilo 60 hadi 90 wakiwa na umri wa miezi sita hadi tisa Nguruwe ana uwezo wa kula vyakula vya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na mabaki ya vyakula vya nyumbani, shambani na viwandani. Pamoja na vyakula hivyo, ni muhimu…
Zalisha mbolea za asili kwa ajili ya kilimo hai
Ili uweze kufanya kilimo hai ni lazima uwe na mbolea za asili. Bila mbolea za asili huwezi kufanya kilimo cha aina yeyote kwa misingi ya kilimo hai. Mbolea za asili zipo za aina mbalimbali ama huweza kutengenezwa kwa njia mbalimbali na kwa kutumia malighafi mbalimbali kama vile samadi, majani ya kurundika nakadhalika. Baadhi ya mbolea za asili na njia za…
Fahamu changamoto zinazosababisha vifo vya samaki katika bwawa
Ufugaji wa samaki kwa sasa ni moja ya mradi mzuri kiuchumi, hapa nchini na nje ya nchi. Pamoja na ufugaji huu kuendelea kuna changamoto zinazoikabili ambazo ni muhimu wafugaji kutambua ili kuepuka hasara. Elimu ya ufugaji wa samaki kwa miaka ya karibuni imekuwa ikiwafikia wengi na hii ni kutokana na usambazaji wa taarifa kwa haraka kwa wafugaji kupitia vyombo mbalimbali…
Wakulima wajidhatiti kudhibiti sumu kuvu msimu wa mavuno
Katika majarida yaliyopita, tuliangazia kwa undani kuhusu sumu kuvu na namna ya kudhibiti. Katika toleo hili tumeona vyema kurudia makala hii hasa kwa kuwa tunaelekea msimu wa mavuno na wakulima wanahitaji kukinga mazao yao na sumu kuvu. Sumu kuvu (Aflatoxin) ni aina za kemikali za sumu zinazozalishwa na aina ya ukungu au fangasi wanaoota kwenye mbegu za nafaka kama vile…
Uzalishaji na utunzaji wa malisho ya mifugo kwa ajili ya kulisha wakati wa kiangazi
Kama wewe ni mfugaji, Je, umewahi kufikiri utalisha vipi mifugo wakati wa kiangazi? Wafugaji walio wengi wanafanya miradi yao bila kuweka mikakati ya upatikanaji wa malisho katika majira yote ya mwaka, hasa kipindi cha kiangazi ambapo upatikanaji wa chakula cha mifugo ni duni. Bila malisho, mifugo haiwezi kuzalisha au kupata uhai. Chakula ni muhimu kwa mifugo kama ilivyo kwa binadamu.…




