- Mifugo

Uzalishaji na utunzaji wa malisho ya mifugo kwa ajili ya kulisha wakati wa kiangazi

Sambaza chapisho hili

Kama wewe ni mfugaji, Je, umewahi kufikiri utalisha vipi mifugo wakati wa kiangazi?

Wafugaji walio wengi wanafanya miradi yao bila kuweka mikakati ya upatikanaji wa malisho katika majira yote ya mwaka, hasa kipindi cha kiangazi ambapo upatikanaji wa chakula cha mifugo ni duni.

Bila malisho, mifugo haiwezi kuzalisha au kupata uhai.

Chakula ni muhimu kwa mifugo kama ilivyo kwa binadamu. Chakula kikuu cha mifugo ni malisho kama vile nyasi, masalia ya mazao, miti, mikundekunde n.k.

Kilimo cha malisho kwa wafugaji husaidia wafugaji kuwa na chakula cha uhakika kwa mifugo yao na kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji na kuboresha ushirikiano wao kwani upungufu wa malisho ni chachu ya migogoro hiyo.

Tafadhali usiache kusoma jarida la Mkulima Mbunifu, toleo lijalo hapa hapa kwenye tovuti yetu.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *