Kumekuwa na tabia ya wafugaji walio wengi kutokuzingatia njia sahihi ya kusafirisha kuku wakati wa kupeleka sokoni au hata kuhamisha toka sehemu moja kwenda nyingine. Hali hii imekuwa ikisababisha mateso pamoja na vifo kwa kuku jambo ambalo pia husababisha hasara. Ni vizuri kuku wakawekwa kwenye tenga au trei yenye nafasi na hewa ya kutosha. Haifai kubananisha kuku kwenye sehemu moja.…
Mifugo
Ubora wa zizi huinua uzalishaji wa mbuzi na kondoo
Ufugaji wa Mbuzi na kondoo ni wa gharama nafuu sana hasa ukilinganisha na ng’ombe kwani wanyama hawa wana uwezo wa kuishi mahali popote na katika mazingira magumu kama yenye maradhi na ukame. Wanyama hawa kulingana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo huku wakihudumiwa na familia zenye nguvu kazi ndogo na kipato cha chini. Wanyama hawa ambao hufugwa…
Ni muhimu kuwa kwenye vikundi ili kupata maendeleo thabiti
Kikundi ni muunganiko wa watu wenye nia/lengo moja katika kutekeleza jambo fulani walilolikusudia kwa faida ya hao walioamua kuwa pamoja. Lengo kuu la kuwa na kikundi ni kutaka kufanya au kutatua tatizo kwa pamoja. Maamuzi ya kikundi kiwenje ikiwa na maana ya ni kikundi cha aina gani na wahusika watakua wangapi hutegemea na lengo kuu la kuunda umoja huo. Kikundi…
Namna bora ya kupambana na maambukizi ya minyoo bapa (Trematodes) kwa mifugo
Aina hii ya minyoo imeripotiwa na wataalamu mbalimbali nchini Tanzania na mahali kwingine duniani kusababisha madhara makubwa kwa mifugo yanayosababisha upotevu mkubwa wa kiuchumi. Minyoo bapa ni minyoo yenye urefu wa kuanzia midogo milimita moja hadi mirefu ya milimita 7. Kinachowatambulisha kwa urahisi ni uwepo wa vifyonzeo vya damu viwili, kimoja kikiwa karibu kabisa na mdomo na kingine kikiwa upande…
Wasemavyo wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu
Mkulima Mbunifu imekua ikitembelea wakulima mbali mbali nchini Tanzania ili kuchukua shuhuda mbalimbali za wanufaika na kuzichapisha ziwe chachu kwa wasomaji wengine kujifunza na kufanya kwa vitendo. Je wewe umejifunza nini kutoka Mkulima Mbunifu? Tafadhali tuandikie kupitia mawasiliano yaliyo katika jarida hili. Katherini Samweli Palanjo, Kijiji cha Sura-Meru, Arusha Mimi ni mkulima wa kilimo hai, ninajishughulisha na kilimo cha mboga…
Utunzaji wa vitoto vya mbuzi na kondoo
Vitoto vya mbuzi na kondoo wanahitaji uangalizi mzuri kwa sababu wao ni mbuzi na kondoo wa kesho. Utunzi mzuri unawafanya kuwa wenye nguvu na afya. Utunzaji wa mbuzi huanza mara tu baada ya kuzaliwa. Mfugaji ahakikishe yafuatayo; Kitoto cha mbuzi/kondoo kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya masaa 24 tangu kuzaliwa na kwa muda wa siku 3. Kama kinanyweshwa maziwa,…
Nguruwe wanahitaji kupata chakula chenye virutubisho sahihi
Nguruwe huhitaji kulishwa vizuri ili waweze kukua haraka na kufikia uzito wa kuchinjwa mapema. Ikiwa watatunzwa vizuri watafikia uzito wa kilo 60 hadi 90 wakiwa na umri wa miezi sita hadi tisa. Nguruwe ana uwezo wa kula vyakula vya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na mabaki ya vyakula vya nyumbani, shambani na viwandani. Pamoja na vyakula hivyo, ni muhimu…
Ukweli kuhusu ufugaji wa ng’ombe wa maziwa
Ikiwa wewe siyo mfugaji wa ng’ombe na unahitaji kufanya hivyo ila unaogopa kulingana na habari toka kwa wafugaji wengine, hebu soma baadhi ya taarifa hizi huenda zikakushawishi kufanya mradi huu kwa furaha na kwa ufanisi zaidi. Unaweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ukiwa na eneo dogo. Unachotakiwa ni kuwa na sehemu inayotosheleza kuwafugia idadi ya ng’ombe ulionao.…
Ni muhimu mkulima kuelewa magonjwa ya mimea
Tafsiri rahisi ya magonjwa ya mimea ni hii: Ni kuwepo kizuizi, au usumbufu fulani unaosababishwa na magonjwa au viumbe fulani kusababisha vichocheo vya ukuaji wa mimea kutokufanya kazi katika hali yake ya kawaida. Kutokana na sehemu ya mmea kupata usumbufu huo, seli za mmea zinaweza kufa au hata kusababisha mmea kufa kabisa. Jambo hili kwa kawaida husababisha kuathirika kwa kiwango…
Tumia mihogo kulisha kuku
Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa nyuzi za mihogo zinaweza kutumika kwa ajili ya chakula cha kuku wanaotaga. Sekta ya kuku hapa Tanzania hutegemea nafaka pamoja na jamii ya kunde kwa ajili ya kutengeneza lishe ya kuku. Nafaka kama vile mahindi, mtama, ngano na shayiri ni chanzo kikubwa cha vyakula vya nguvu katika ulishaji wa kuku. Jamii ya kunde kama…






