- Mifugo

Usisafirishe kuku kwa kuwarundika au kuning’iniza kichwa chini

Sambaza chapisho hili

Kumekuwa na tabia ya wafugaji walio wengi kutokuzingatia njia sahihi ya kusafirisha kuku wakati wa kupeleka sokoni au hata kuhamisha toka sehemu moja kwenda nyingine. Hali hii imekuwa ikisababisha mateso pamoja na vifo kwa kuku jambo ambalo pia husababisha hasara.

Ni vizuri kuku wakawekwa kwenye tenga au trei yenye nafasi na hewa ya kutosha. Haifai kubananisha kuku kwenye sehemu moja. Hali hiyo inaweza kusababisha kuku hao kufa na kumsababishia mfugaji hasara.

Jambo la muhimu na la msingi ni kuzingatia idadi ya kuku unaohitaji kupeleka sokoni na kuandaa mazingira mazuri ya kusafirisha ili wafike salama na kuepuka hasara inayoweza kutokea kutokana na usafirishaji usio sahihi.

Kama alivyo binadamu, ndivyo ambavyo wanyama na ndege wote wanahitaji kuthaminiwa na kutengwa mbali na mateso yanaweza kuwapelekea kuumia na hata kufa.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *