- Mifugo

Karibu maonyesho ya Nane Nane 2020

Sambaza chapisho hili

Kama ilivyo ada kila mwaka nchini Tanzania, wakulima hujumuika pamoja kusherehekea wiki ya kitaifa ya kilimo ambayo hufanyika kikanda nchini Tanzania.

Maonyesho hayo mahususi hutoa fursa kwa wakulima kufahamiana na kuonesha bunifu mbalimbali, nyenzo za kilimo, usindikaji na masoko ya bidhaa mbalimbali za kilimo.

Mwaka huu maonyesho hayo yatafanyika kitaifa mkoani Simiyu, Mkulima Mbunifu itashiriki kikamilifu hivyo usiache kututembelea katika banda letu.

Katika maonyesho haya ya nane nane kanda ya kaskazini Mkulima Mbunifu itashirikiana na wadau wengine wa kilimo hai, kama shamba la kilimo hai la St Joseph wakifundisha na kueleza bidhaa mbalimbali za kilimo hai ambazo zitapatikana kwenye banda hivyo karibu ujifunze mengi kutoka kwa wakulima wabunifu wa kilimo hai.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *