Ni muhimu kusindika viazi vitamu ili kuongezea thamani, ubora na matumizi yake Viazi vitamu husindikwa kupata viazi vitamu vilivyokaushwa, unga, wanga na jamu. Ukaushaji wa viazi vitamu kwa ujumla wake huhitaji au hutumia nishati ya jua ambapo ni lazima mkulima kuzingatia kanuni kwa ajili ya kukausha mazao yake. Kanuni muhimu za ukaushaji Ukaushaji hupunguza maji kwenye zao la viazi vitamu…
Mifugo
Unawezaje kutambua mnyama mwenye afya nzuri na mwenye matatizo ya kiafya?
Afya ya mifugo ni tatizo kubwa linalowakabili wafugaji walio wengi katika sehemu mbalimbali za nchi. Wapo wataalamu mbalimbali katika maeneo na mikoa yote ya nchi wanaotoa huduma ya mifugo lakini, bado kuna changamoto nyingi zinazowakumba wafugaji. Katika sehemu ambazo mawasiliano ikijumuisha pia miundo mbinu kuwa duni, wafugaji wamekuwa wakipoteza mifugo hasa kutokana na sababu kuwa mara ugonjwa unapoikumba inakuwa si…
Fahamu maandalizi muhimu kabla ya nguruwe kuzaa
Nguruwe wanaozaa kwa mara ya kwanza wanaweza kupelekwa kwenye nyumba ya kuzalia masaa machache kwa siku kutoka siku kumi kabla ya siku ya kuzaa ili waweze kuzoea mazingira. Mara nyingi tumekuwa na makala zinazoelezea ufugaji wa nguruwe katika nyanja tofauti, ikiwa ni pamoja na aina, matunzo na magonjwa ya nguruwe na hata bidhaa zinazotokana na nguruwe na usindikaji wake. Katika…
Shubiri mwitu (aloe) tiba ya magonjwa ya kuku
Kuku ni moja ya miradi inayofanywa kwa wingi na watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wakulima na wafugaji, na wanaofanya shughuli nyinginezo. Moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili na kuzungumziwa mara kwa mara ni magonjwa yanayoshambulia kuku, bila wafugaji kufahamu ni nini cha kufanya. Kumekuwepo na njia mbalimbali za kutibu kuku, zikiwemo za asili na zisizokuwa za asili. Moja wapo ya…
Nyuki wadogo: Mjasiriamali asiyekuwa na gharama wala madhara
Ninataka kufuga nyuki wadogo, kwa kuwa nasikia wana faida kubwa sana, lakini sijui namna ya kuwapata na jinsi ya kuwatunza, naombeni msaada-Msomaji MkM Nchini Tanzania na maeneo mbalimbali barani Afrika, imekuwa ni mazoea kwa wanaotaka kufanya ufugaji wa nyuki kufuga nyuki wakubwa au maarufu kama nyuki wakali. Aina hii ya nyuki imekuwa ni rahisi kufugwa kwa kuwa uzalishaji wake ni…
Ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine
Katika ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine mambo kadha wa kadha ni muhimu sana kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kujua aina ya samaki wanaofaa kufugwa, faida za mboga na hata mifugo mingine kama kuku wanaojumuishwa katika ufugaji huu. Aina ya samaki wanaofaa katika kilimo mseto Perege na Kambale ni samaki wanaofugwa katika maeneo mabalimbali nchini Tanzania. Perege ndiyo aina…
Tumia dawa za asili zinazopatikana katika maeneo ya wafugaji kutibu magonjwa mbalimbali ya mifugo
Yapo magonjwa mbalimbali ambayo mfugaji hasa aliyeko kijijini anaweza kuyatibu kwa kutumia dawa za asili ambazo pia zainapatikana katika maeneo yao bila hata kutumia dawa za madukani. Faida ya kutumia dawa hizi ni kubwa kwani husaidia kuokoa maisha ya mfugo kwa haraka zaidi kama huduma ya madaktari iko mbali, hupunguza gharama za kununua dawa pamoja na kumlipa afisa mifugo. Mimea…
Uandaaji na uoteshaji wenye tija wa miche ya vanila
Vanila ni zao la biashara ambalo asili yake ni mexico zao hili limekua likilimwa na kuzalishwa huko mexico, marekani na bara Hindi kwa karne nyingine. Hivi sasa, zao hili linalimwa maeneo mengi barani Afrika ikiwamo nchi ya Tanzania, japo kwa uchache kutokana na ugumu wake wa kulizalisha, ingawa bei yake ni kubwa sana na wakulima waliofanikiwa kuzalisha wamekuwa wakipata kipato…
Gliricidia: Mti wenye faida lukuki kwa mkulima
Gliricidia ni mti ambao kisayansi hujulikana kwa jina la gliricidia sepium ambao hutumika kwa ajili ya mbolea au kurutubisha ardhi. Mti huu wa gliricidia ni jamii ya miti ya malisho ambayo majani yake hutumika kurutubisha udongo na kulishia mifugo hasa katika kipindi cha ukame. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kumudu kuzalisha wakati wa kiangazi pamoja na kudumisha hali…
JAGEF wanaonesha njia katika usindikaji wa vyakula
“Kukaa mwenyewe na kufanya shughuli za ujasiriamali ni rahisi sana kuanguka, kutokutambuliwa au kuweza kupiga hatu, lakini mkiwa kwenye kikundi, mnapiga hatua kwa haraka sana na wepesi zaidi” Ndivyo alivyoanza kueleza mama Ester Moshi, mwenyekiti wa kikundi cha wasindikaji cha JAGEF katika kijiji cha Kikarara Old Moshi mkoani Kilimanjaro alipokuwa akielezea shughuli za kikundi hicho. JAGEF kilianza mwaka 2010 kikiwa…