Sadick Amri anauliza: Naomba niulize utalijuaje yai lenye uwezo mkubwa wa kutotolewa. Mwang’oko Milamo anajibu: Yai lolote lililotagwa na kuhifadhiwa katika mahala pasafi, bila kushikwa shikwa na mikono yenye mafuta, na kufanya yai lipungue, hutotolewa. Aidha yai lililotagwa na kuku aliyelishwa aliyepata lishe kamili, kuku waliopata ratio nzuri kati yao na majogoo, yai lililotagwa na kuku asiye na matatizo ya…
Mifugo
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…
Gugu karoti lina madhara makubwa
Gugu karoti (Parthenium hysterophorus) ni mmea vamizi ambao una madhara mengi kwa binadamu, mazao, wanyama au mifugo pamoja na kuharibu uoto wa asili. Gugu hili lina madhara mengi kama; Muwasho unaoweza kusababisha kujikuna na kupata malengelenge, ugonjwa wa pumu ukivuta vumbi lake, muwasho wa macho, mnyama kupasuka na kuvimba midomo kama akila majani. Aidha gugu karoti husababisha maziwa ya ng’ombe…
Ustawishaji wa malisho ya nyasi na mikunde kwenye makingo
Ni muhimu kwa wafugaji kutumia makingo katika kuzalisha malisho aina ya nyasi na mikunde ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malisho bora na ya kutosha. Makingo hutengenezwa kwa kuchimba mitaro na kupanda majani kwenye mistari ya kontua. Makingo pia huweza kutengenezwa kwa kutumia mawe, takataka au mabaki ya shambani baada ya mavuno. Umuhimu wa makingo Makingo yanahitajika sana…
Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa
Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kisayansi kwa jina la Phlebovirus vya kabila la Bunyaviridae. Virusi hivi huenezwa na wadudu waumao hasa mbu wa aina ya Aedes, Anopheles, Culex, Mansonia nk. Ugonjwa huu huwapata ng’ombe, mbuzi, ngamia, kondoo na pia binadamu. Ugonjwa huu pia huwapata wanyamapori kama vile; swala, nyati na nyumbu. Njia…
Mambo machache muhimu ya kuzingatia kwa uzalishaji wa ng’ombe
Kuna aina nyingi za chanjo, na chanjo hizo zimegawanyika katika makundi mawili, chanjo hai na chanjo mfu. Chanjo mfu inabidi irudiwe kila mwaka au zaidi kulingana na aina ya ugonjwa. Chanjo hai huchomwa mara moja kwa mwaka au miaka mitatu kisha kurudiwa tena. Chanjo hizi hutolewa kwa ajili ya magonjwa yanayosababishwa na bakteria na virusi. Magonjwa menghine kama ECF hayana…
Nguruwe: Mifugo yenye gharama ndogo, tija zaidi
Kwa kawaida nguruwe ni lazima wafugwe ndani ya banda, wasiachwe kuzurura ovyo nje Ili kuwa na ufugaji wenye tija, na kuweza kuepuka baadhi ya magonjwa yanayoshambulia nguruwe, ni lazima mfugaji azingatie mambo ya msingi katika ufugaji. Banda Ni muhimu kuhakikisha kuwa unapohitaji kufuga nguruwe, unakuwa na banda lililotayarishwa vizuri na liwe imara. Utayarishaji mbaya wa banda unaweza kusababisha nguruwe kuugua…
Nawezaje kutunza g’ombe na kukabilina na magonjwa
Bila matunzo mazuri na kuzingatia kanuni za ufugaji, mfugaji hawezi kupata faida na kufikia malengo yake. Shauriana na wataalamu unapoona kuna jambo linalokutatiza Ufugaji hasa wa ng’ombe wa maziwa ni shughuli ambayo imejipatia umaarufu kwa kiasi kikubwa sana katika jamii mbalimbali, maeneo ya vijijini na hata mijini. Pamoja na shughuli hii kuwa maarufu na yenye faida, kuna changamoto mbalimbali zinazoambatana…
Wanahabari na Kilimo hai
Siku za hivi karibuni, mradi wa Mkulima Mbunifu uliratibu na kuendesha mafunzo ya kilimo hai kwa waandishi wa habari nchini Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tatu yalifanyika katika shamba la kilimo hai SJS- St Joseph Sustainable Organic Farm lililopo katika kijiji cha Kwanyange Wilaya ya Mwanga. Mafunzo haya yalifadhiliwa na shirika la Biovision (Bv) Foundation lililopo Switzerland. Katika mafunzo hayo…
Utunzaji bora wa majike ya nguruwe
Utunzaji bora wa majike ni muhimu kwani utamuwezesha mfugaji kupata mazao mengi na bora. Majike wazazi watunzwe vizuri ili kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa kwa mwaka na kuongeza faida kwa mfugaji. Utunzaji bora ni kiini cha idadi ya watoto watakaozaliwa,watakaoishi na Muda wataochukua kufikia uzito kuuza na gharama zitakazotumika. Kuchagua jike bora Mfugaji anashauriwa kuchagua nguruwe jike anayetegemewa kuwa mzazi…