Kutuhusu
Kwa nini tunafanya kilimo?
Kilimo kimekuwepo tangu kale za mababu zetu. Binadamu wa kwanza walipata chakula chao kwenye mazingira yanayowazunguka na kwa juhudi kama uwindaji kabla ya kuanza kulima ardhi, kupanda mazao na kufuga mifugo kama vyanzo vya lishe. Hii ni pamoja na nafaka, mazao ya mizizi, karanga, matunda, nyama, maziwa, na hata mayai. Kilimo kimebadilisha maisha na maisha pia yamebadilisha muundo wa kilimo.…
Uboreshaji na usambazaji wa habari za kilimo
Kwa miaka iliyopita, Mkulima Mbunifu iliweza kufanya mafunzo mbalimbali, kwa waandishi wa habari, maafisa kilimo na mifugo, lengo likiwa ni kuongeza uelewa pamoja na kufundisha mbinu mbalimbali za kuandika makala zinazohusu kilimo endelevu, na namna ya kutumia vyombo vya habari katika kufundisha juu ya kilimo endelevu. Washiriki katika semina mbalimbali zilizofanyika, walitoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwepo Tabora, Iringa, Dar…