- Kutuhusu

Umuhimu wa shamba darasa katika kilimo hifadhi

Sambaza chapisho hili

Kwanza, tujiulize shamba darasa ni nini? Hiki ni kikundi cha wakulima kati ya 20-25 wenye tatizo linalofanana waliokubaliana kutatua kwa pamoja wakiwa na mwezeshaji wao kwa kupata ufumbuzi endelevu. Vile vile, waweza kusema shamba darasa ni shule bila ukuta inayohusisha wakulima kati ya 20-25 waliokuba-liana kutatua tatizo lao kwa pamoja, na mafunzo yote hufanyika shambani.

Matatizo ya shambani yanachungu-zwa na kupatiwa ufumbuzi toka wakati wa kupanda hadi kuvuna, hivyo wakulima hufanya zoezi hili kwa vitendo katika shamba lao la majari-bio kwa msimu mzima. Wanajifunza kwa vitendo, wanachunguza nini kinatokea, wanafanya tathmini na wanaorodhesha kwa umuhimu teknolojia ambazo wanaona zita-wafaa.

Kuongezea, huwa na masomo maalum yaliyopendekezwa na wa-nakikundi wenyewe wapatiane, hivyo kuwafanya wakulima kujiamini katika kufanya maamuzi na kuendeleza ubunifu wao kwa kilimo endelevu.

Tofauti ya shamba darasa na vikundi vingine

  • Hutoa fursa huru na shirikishi ya kujifunza.
  • Huwawezesha wakulima kufanya maamuzi wenyewe kwa uhakika
  • Hueneza teknolojia kwa watu we-ngi na haraka.
  • Ni sehemu ya pamoja ya kujifunzia
  • Huwezesha teknolojia nyingine kufundishwa.
  • Kujifunza kwa vitendo na kugundua matatizo ya kile wanachochunguza wenyewe.

Kwa nini shamba darasa

  • Kupunguza gharama za kueneza teknolojia.
  • Kutoa fursa huru na shirikishi ya wakulima, hivyo huzalisha wakulima wawezeshaji wengi.
  • Kuongeza fursa ya wakulima kuku-tana na mwezeshaji/mgani hivyo kupunguza gharama ya uenezi wa teknolojia.
  • Kurahisisha kazi ya ugani badala ya kuwatembelea kila kaya kwa siku 25.

Lengo kuu la shamba darasa

  • Kuongeza uzalishaji kwa eneo.
  • Kupunguza gharama za uzalishaji.
  • Kuwawezesha wakulima kufanya maamuzi kwa uhakika.
  • Kutoa fursa huru na shirikishi ya kujifunza.

Kanuni za shamba darasa

  • Kukuza mimea yenye afya.
  • Kuhifadhi wadudu marafiki.
  • Kukagua shamba mara kwa mara.
  • Mkulima kuwa mtaalamu katika shamba lake.

Hatua za kuanzisha na kuendesha shamba darasa

  • Mafunzo kwa wawezeshaji ugani na wakulima wachache.
  • Maandalizi ya awali – hii inaju-muisha kuona uongozi wa kijiji ili kuomba kukutana na kuongea na wakulima, kujadili, kupata matatizo na mapendekezo ya ufumbuzi
  • Majaribio ya teknolojia zilizocha-guliwa.
  • Tathmini ya teknolojia zilizo ja-ribiwa (tathmini, pata maana yake na wasilisha).
  • Siku ya wakulima – siku hii ni maa-lum maana inatambua rasmi muda uliotumika. Pia, ni sehemu ambayo inatumika kueleza wakulima na watu wengine walichojifunza kwenye shamba darasa. Hii inachochea hamasa kwa wengine ili msimu ujao wajiunge au waa-nzishe mashamba darasa yao.

Mara nyingi, siku ya wakulima ina-tayarishwa na wakulima wenyewe wakisaidiana na afisa ugani wao. Pia, mavuno na matokeo ya shamba yanaonyeshwa, mara nyingine wanaonyesha matokeo ya walichojifunza.

  • Hitimisho – inafanywa mwisho wa msimu kuonyesha mwisho wa mafunzo na kuwashukuru wakulima kwa muda wao waliotumia kuji-funza ili wawe wataalamu.
  • Shamba darasa zinaendeshwa na wakulima.
  • Ufuatiliaji wa mashamba darasa yanayoendeshwa na wakulima.

KUMBUKA: Watu wanakumbuka asilimia 20 ya kile wanachosikia, asilimia 40 ya wanachoona, na asilimia 80 ya wanachogundua au kufanya wao wenyewe.

 Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr. Benjamini Rwambano (Bwana Shamba) Arusha – 0754025113.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *