Kilimo

- Kilimo

Kilimo mseto na utunzaji wa mazingira

Mara nyingi wafugaji wa mbuzi na hata wale wa wanyama wengine huendesha pia shughuli za kilimo. Katika mashamba yao ya mazao huotesha pia mimea ya aina nyingine, hii ikiwa ni pamoja na miti. Kilimo mseto ni mfumo wa kilimo wa kuchanganya miti na mazao katika shamba moja. Miti sahihi kwa kilimo mseto humnufaisha mfugaji kwa njia nyingi. Miti hiyo huweza…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mazingira

Madhara yatokanayo na uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO uchafuzi wa mazingira husababisha takribani vifo milioni saba (7) kila mwaka, na kusababisha ulemavu kwa watu wanaoishi na magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa hewa.   Nini sababu za uchafuzi wa hali ya hewa Uchafuzi wa hewa husababishwa na gesi na chembechembe zinazoruhusi­wa kuingia angani kupitia shughuli mbalimbali za kibinadamu. Miongoni mwa shughuli…

Soma Zaidi

- Kilimo

Uzalishaji wa kilimo hai (TAZAMA VIDEO)

Mazao ya kilimo hai Kilimo hai ni aina ya kilimo ambacho hakitumii mbolea wala dawa za viwandani katika uzalishaji wake wa mazao. Mazao yanayozalishwa kwa kutumia kilimo hiki huwa na bei ya juu sana kutokana na kuwa ni salama kwa afya ya mtumiaji. Mazao hayo hayana madhara ya muda mfupi wala mrefu hivyo mtumiaji hana hofu kupatwa na magonjwa.

- Kilimo

Wafahamu nzige na jinsi ya kuwadhibiti

Nzige huvamia bustani, shamba na ana uwezo wa kuharibu vibaya kabisa. Katika (matukio mengi) nzige hudhibitibiwa na viuatilifu ambazo ni kemikali sumu za kuua wadudu, ambazo si rafiki na mazingira kwani vinauwezo wa kuua viumbe wengine, pia hatari kwa binadamu. Kutumia hatua mbadala na asili kusaidia kudhibiti idadi yao ni vema. Nzige wa jangwani ni miongoni mwa wadudu wa aina…

Soma Zaidi

- Kilimo

Udhibiti wa wadudu kwenye zao la mihogo

Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu. Kilimo cha zao la mhogo, kama ilivyo kwa mazao mengine ya mizizi, kina­zongwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wadudu na magonjwa ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiasi cha mavuno,…

Soma Zaidi

- Kilimo

Uvunaji na uhifadhi bora wa mazao ya nafaka

Nafaka mbalimbali ambayo ni mazao makuu ya chakula na kibiashara hapa nchini kama vile mahindi, maharage, mikunde mara nyingi wakulima hupoteza hasa wakati wa mavuno kutokana na uvunaji usiokidhi viwango pamoja na uhifadhi duni. Ukiwa huu ni msimu wa mavuno katika maeneo mbalimbali nchini, Mkulima Mbunifu inatoa rai kwa wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni sahihi za mavuno ili waweze kupata…

Soma Zaidi

- Kilimo

Amrut Jal! kioevu cha udongo na kirutubisho cha kikaboni

Kama ilivyo kwa mwili wa binadamu unahitaji chakula chenye virutubisho, vivyo hivyo udongo wa kikaboni pia unahitaji kurutubishwa ili uweze kuzalisha vizuri. Amrut Jal ni mbolea ya kioevu cha kikaboni ambacho huimarisha kiwango cha virutubisho katika udongo unaotumika kwa kilimo hai. Mkulima hana budi kujifunza namna ya kutengeneza na kutumia Amrut Jal katika shamba la kilimo hai. Jinsi ya kutengeneza…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo, Mimea, Redio, Usindikaji

Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu

Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo, Mimea, Redio, Usindikaji

Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo

Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mimea, Udongo

Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea

Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu. Hii ni hali ya kimaumbile katika kusawazisha idadi. Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuzidi idadi na kusababisha madhara. Madhumuni ya njia ya kiasili…

Soma Zaidi