- Kilimo

Zalisha mbolea za asili kwa ajili ya  kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Ili uweze kufanya kilimo hai ni lazima uwe na mbolea za asili. Bila mbolea za asili huwezi kufanya kilimo cha aina yeyote kwa misingi ya kilimo hai.

Mbolea za asili zipo za aina mbalimbali ama huweza kutengenezwa kwa njia mbalimbali na kwa kutumia malighafi mbalimbali kama vile samadi, majani ya kurundika nakadhalika.

Baadhi ya mbolea za asili na njia za kuzalisha mbolea za asili ambazo mkulima wa kilimo hai huweza kutumia katika kilimo kwa ajili ya uzalishaji bora ni pamoja na mabaki ya mazao, mazao funikizi, matandazo, samadi ya ng’ombe na mboji.

Mbolea za asili zina faida kuu mbili, moja huongeza na kushamirisha viumbe hai katika udongo na pia ni huru kwani unaweza kuotesha au kutengeneza mwenyewe. Na pia kama utakuwa na mbolea nyingi kupita mahitaji yako, unaweza kuuza na ikanunuliwa.

Hata hivyo baadhi ya mbolea za asili zinakosa kirutubisho muhimu cha kutosha cha fosiforasi ambayo mmea huhitaji kwa ajili ya kukua. Hata hivyo, unaweza kuongeza ubora wa mbolea za asili kwa kuongeza mimea yenye virutubishi vya fosifirasi kwa wingi.

Mabaki ya mimea

Mabua na majani ya baadhi ya mazao ni mazuri sana kwa matandazo. Stover kutoka kwenye mahindi na mtama huanza kuoza taratibu nhivyo hukaa juu ya ardhi kwa muda mrefu kido na kufanya kufunika udongo.

Aidha, mabua na majani ya mikundeyana wingi wa naitrojeni na huoza kwa haraka hivyo kuwezesha virutubishi kutumika kwa haraka kwa mimea itakayofuata kuoteshwa.

Mazao funikizi

Mazao funikizi yanahitajika kuoteshwa mapema yakiwa yanafaa katika mseto wa kilimo hivyo kuwezesha kukua na kufunika udongo.

Baada ya kuota, yafyeke na kuacha juu ya ardhi kama masalia kabla ya kuotesha zao kuu linalofuata.

Mazao funikizi jamii ya mikunde ni muhimu sana kwa zinakusanya naitrojeni kutoka hewani na kuifanya kutumika kwa mazao mengine.

Nyasi na magugu

Unaweza kukata na kukusanya nyasi na magugu kutoka pembezoni mwa shamba au kutoka katika eneo lingine na kuyatandaza shambani kama matandazo, lakini kwa kufanya uangalifu mkubwa ili usichukue yenye mbegu kwani baadaye huota na kusababisha kuwepo kwa magugu shambani.

Kupogoa majani kutoka kwenye miti na vichaka

Unaweza kupogoa majani ya miti na vichaka ulivyovikata kisha kuweka kama matandazo. Miti na vichaka jamii ya mikunde ni mizuri zaidi kwakuwa zina kiwango kikubwa cha naitrojeni na unaweza kuvuna vichaka katika kipindi chochote cha mwaka.

Aidha, baadhi ya mimea huoza haraka wakati mingine ikichukua muda kidogo hivyo ni muhimu kutumia aina mbalimbali ya mimea ili kupata mchanganyiko mzuri wa kufunika udongo na uweze kuozesha mimea kwa haraka wakati utakapohitaji.

Kinyesi cha wanyama (samadi)

Samadi inayotokana na kinyesi cha wanyama ni mbolea nzuri sana katika kilimo hai. Aidha, baada ya kukusanya kinyesi hiki kutoka kwa wanyama, iachwe ili iweze kuoza kabla ya kupeleka shambani kwani ukiweka moja kwa moja ikiwa imetoka kwa wanyama ikigusa mimea huweza kuunguza.

Kinyesi kinachotokana na kuku hutengeneza pia mbolea nzuri sana kwa ajili ya kilimo hai ikifuatiwa na kinyesi cha mbuzi, kondoo na kinyesi cha ng’ombe.

Mboji

Unaweza kutengeneza mboji kutokana na majani, magugu, samadi, majivu, uchafu kutoka jikoni au malighafi yeyote ya asili yanayopatikana katika eneo lako.

Wakati wa kutengeneza mboji, jaribu kutumia malighafi inayooza haraka na kuzalisha mboji mapema kama vile nyasi na majani.

Unaweza pia ukatengeneza mboji kwa kuweka malighafi kwenye shimo hasa katika maeneo yenye mvua kidogo au za wastani.

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *