Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu. Kilimo cha zao la mhogo, kama ilivyo kwa mazao mengine ya mizizi, kinazongwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wadudu na magonjwa ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiasi cha mavuno,…
Kilimo
Uvunaji na uhifadhi bora wa mazao ya nafaka
Nafaka mbalimbali ambayo ni mazao makuu ya chakula na kibiashara hapa nchini kama vile mahindi, maharage, mikunde mara nyingi wakulima hupoteza hasa wakati wa mavuno kutokana na uvunaji usiokidhi viwango pamoja na uhifadhi duni. Ukiwa huu ni msimu wa mavuno katika maeneo mbalimbali nchini, Mkulima Mbunifu inatoa rai kwa wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni sahihi za mavuno ili waweze kupata…
Amrut Jal! kioevu cha udongo na kirutubisho cha kikaboni
Kama ilivyo kwa mwili wa binadamu unahitaji chakula chenye virutubisho, vivyo hivyo udongo wa kikaboni pia unahitaji kurutubishwa ili uweze kuzalisha vizuri. Amrut Jal ni mbolea ya kioevu cha kikaboni ambacho huimarisha kiwango cha virutubisho katika udongo unaotumika kwa kilimo hai. Mkulima hana budi kujifunza namna ya kutengeneza na kutumia Amrut Jal katika shamba la kilimo hai. Jinsi ya kutengeneza…
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Njia za asili za kukabiliana na wadudu na magonjwa katika mimea
Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu. Hii ni hali ya kimaumbile katika kusawazisha idadi. Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuzidi idadi na kusababisha madhara. Madhumuni ya njia ya kiasili…
Utengenezaji wa mbolea ya mboji kwa mazao ya kilimo hai
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Vipande vya vitu au sehemu za viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda…
Matumizi ya Molasi na faida zake kwa uzalishaji wa mazao
Katika kilimo, matumizi ya Molasi ni muhimu kwa kuboresha hali ya udongo, kudhibiti wadudu, kuwezesha udongo kuwa na rutuba, kurekebisha hali ya udongo na pia kupunguza matatizo kwa mimea inayopandikizwa. Matumizi ya Molasi husaidia kusafisha mipira ya umwagiliaji lakini pia utafiti unaonyesha kuwa Molasi husaidia kuboresha ubora wa udongo. Matumizi na kiasi cha kutumia Kuboresha umbile la udongo. Molasi…
Zao lenye faida kubwa kiuchumi na kiafya
Nanasi ni moja kati ya matunda ambayo yanapendwa sana na watu wa kada zote. Tunda hili halihitaji gharama kubwa ya uzalishaji, huku likiwa na bei nzuri tofauti na ilivyo kwa aina nyinginezo za matunda. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi, Zanzibar na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa…
Mkulima Mbunifu inazidi kupenya katika vijiji kuwafikia wakulima wadogo
Mhariri wa jarida la Mkulima Mbunifu Erica Rugabandana (Wa kwanza kulia waliosimama) baada ya kutembelea kikundi cha wakulima wanufaika wa jarida la MkM wilayani Lushoto