Kilimo

- Kilimo

Fuata kanuni sahihi za kilimo upate mavuno bora

Wakulima walio wengi wamekuwa wakijikita zaidi katika matumizi ya mbolea    ili kupata matokeo mazuri katika kilimo,  na kusahau kuwa kanuni bora za uzalishaji pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka na kupatikana kwa mavuno yenye ubora. Nini cha kuzingatia ili kupata mavuno bora Ni lazima mkulima kufuata utaratibu wa uzalishaji wa mazao katika kila msimu wa kilimo. Hatua zifuatazo ni lazima…

Soma Zaidi

- Kilimo

Utupa: Mmea wa ajabu unaofaa kwa matumizi mengi

Utupa ni aina ya mmea unaopatikana zaidi sehemu zenye baridi hasa nyanda za juu na unastawi sehemu zenye mvua za wastani na nyingi. Mmea huu hauhimili ukame. Utupa hukua haraka na kusambaa kama usipodhibitiwa, baadhi ya nchi mmea huu umepigwa marufuku kupanda kwa sababu ya kutishia uoto wa asili. Matumizi Kufukuza panya / mchwa Mmea wa utupa ni moja ya…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Wanafunzi washirikishwe katika masuala ya kilimo

Shule ya Sekondari Shambalai ‘‘Tuna furaha sana kukutana na Mkulima Mbunifu katika utoaji wa elimu kwani tuna bustani yetu tuliyoianzisha kwa msaada wa mwalimu mkuu, na tumeshindwa kuiendeleza kwa muda mrefu sasa kulingana na kuwa kila tulichokuwa tukijaribu kuotesha tulikosa mavuno lakini jarida hili limetupa nguvu ya kuanza kwa upya.’’ Hayo ni maneno ya mmoja wa wanafunzi wa shule hii…

Soma Zaidi

- Kilimo

Wakulima wazidi kutoa shuhuda

Loseriani Sikayoni: “Nimepungunza ujinga kwa kiasi kikubwa baada ya kusoma jarida la Mkulima Mbunifu. Nimejua namna ya kufanya kilimo cha mzunguko, natunza mifugo yangu kisasa, faida ni kubwa.” Ndivyo alivyoanza kusema mzee Loseriani Sikayoni mkulima kutoka kijiji cha Ilkiding’a, mkoa wa Arusha. Kwa miaka mingi, mzee huyu amekuwa akifanya shughuli za kilimo, na maisha yake kwenda vizuri; ikiwa ni pamoja…

Soma Zaidi

- Kilimo

Maji moto (weaver’s ant) wadudu rafiki wanaowezesha kilimo hai

Maji Moto au Sangara ni aina ya wadudu, ambao ni rafiki kwa mkulima yeyote anayefanya shughuli zake kwa kuzingatia misingi ya kilimo hai. Ni wadudu wadogo sana ambao huishi katika miti ya mikorosho pamoja na miembe. Mara nyingine hupatikana pia katika pamba. Ikumbukwe kuwa tangu kuumbwa dunia, kila kitu kilikuwa kiasili, watu walikula vyakula na matunda ambayo yalikuwa katika mfumo…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mimea

Samadi ya wanyama na mimea

Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni. Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho. Samadi iliyo tayari kwa matumizi Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mimea

Mapapai bora hupelekea soko lenye tija

Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamin A na madini ya kalsiamu kwa wingi na zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini kwa wastani wa tani 2,582 kwa mwaka. Ili kuweza kuzalisha zao la papai kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa ni muhimu kuhakikisha unazingatia kanuni zote za kilimo bora za uzalishaji wa mapapai. Ubora…

Soma Zaidi

- Kilimo

Jifunze namna bora ya ubebeshaji wa miche ya matunda mbalimbali

Ubebeshaji maana yake ni uunganishaji wa sehemu mbili au zaidi za mimea tofauti na kuwa mmea wenye shina moja. Ubebeshaji hufanyika katika mimea ya mazao ambayo yako katika jamii au ukoo mmoja kwa mfano; embe dodo na viringe, chungwa na limao, parachichi aina ya hass na la kienyeji, passion zambarau na njano, biringanya za aina tofauti, maua ya waridi ya…

Soma Zaidi