Soko ni mahali au njia ambayo muuzaji na mnunuzi hukutana na kubadilishana mali au huduma. Ni fursa ya kuuaza na kununua. Kwa kawaida tunapozungumzia soko, tunagusia mambo kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na ukubwa wake, yaani wingi wa wauzaji na wanunuzi katika soko husika, ushindani, washindani, bidhaa na bei zake, changamoto, pamoja na mabadiliko yanayotegemewa. Kwa upande mwingine, tunaweza…
Kilimo
Wakulima kuweni makini na mbegu feki
Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (Tosci), inaendelea kutoa nafasi kwa wakulima kupata elimu ya kutosha kuhusiana na mbegu bora. Wakulima wanaaswa kuachana na mfumo uliopo wa kuthamini mbegu kutoka nje ya nchi, na badala yake wathamini mbegu zinazozalishwa nchini kwa faida yao na vizazi vijavyo. Halikadhalika wakulima watoe taarifa haraka kwenye taasisi hiyo pindi wanaposhtukia uwepo wa mbegu…
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…
Gugu karoti lina madhara makubwa
Gugu karoti (Parthenium hysterophorus) ni mmea vamizi ambao una madhara mengi kwa binadamu, mazao, wanyama au mifugo pamoja na kuharibu uoto wa asili. Gugu hili lina madhara mengi kama; Muwasho unaoweza kusababisha kujikuna na kupata malengelenge, ugonjwa wa pumu ukivuta vumbi lake, muwasho wa macho, mnyama kupasuka na kuvimba midomo kama akila majani. Aidha gugu karoti husababisha maziwa ya ng’ombe…
Sindika machungwa kuepuka hasara na upotevu usio wa lazima
Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa sana kwa wingi katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Mwanza. Zao hili ni la chakula na biashara. Ikiwa huu ni msimu wa machungwa, wakulima hawana budi kujifunza namna mbalimbali za kusindika zao hili ili kuondokana na upotevu unaotokana na wingi wake na kukosekana kwa soko…
Ni muhimu kuelewa magonjwa ya mimea
Tafsiri rahisi ya magonjwa ya mimea ni hii: Ni kuwepo kizuizi, au usumbufu fulani unaosababishwa na magonjwa au viumbe fulani kusababisha vichocheo vya ukuaji wa mimea kutokufanya kazi katika hali yake ya kawaida. Kutokana na sehemu ya mmea kupata usumbufu huo, seli za mmea zinaweza kufa au hata kusababisha mmea kufa kabisa. Jambo hili kwa kawaida husababisha kuathirika kwa kiwango…
Wanahabari na Kilimo hai
Siku za hivi karibuni, mradi wa Mkulima Mbunifu uliratibu na kuendesha mafunzo ya kilimo hai kwa waandishi wa habari nchini Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tatu yalifanyika katika shamba la kilimo hai SJS- St Joseph Sustainable Organic Farm lililopo katika kijiji cha Kwanyange Wilaya ya Mwanga. Mafunzo haya yalifadhiliwa na shirika la Biovision (Bv) Foundation lililopo Switzerland. Katika mafunzo hayo…
Zingatia haya kabla ya kuanza kilimo hai
Wakulima wengi wamekuwa wakitamani kufanya uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai na hata wengine wakiwa tayari wanazalisha lakini wakikwama kutokana na mambo kadha kama kukosa soko, mazao kuharibika au kukosa elimu sahihi ya uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai. Wakulima wengi wanakata tamaa kwa kushindwa kufikia malengo huku wengine wakiacha kabisa uzalishaji wa kilimo hai. Ili uweze kuzalisha kwa usahihi…
Tumia Azola kama mbolea katika kilimo hai
Azola ni majani au magugu ambayo huota sehemu yenye maji kwa wingi. Mmea huu umekua ukitumiwa zaidi na wafugaji wengi kama chakula mbadala kwa kuku. Huweza kuliwa na kuku ikiwa mbichi au fresh au ukivunwa na kuanikwa kisha kuchanganywa kwenye chakula cha kuku. Majani haya huweza kutumika kulisha mifugo mingine kama vile bata, ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kondoo, sungura na pia…
Akiri kilimo hai kimemsaidia kuwa maarufu na kujikwamua kiuchumi
Mkulima Mbunifu hutembelea wakulima wa kilimo hai popote walipo kujifunza na kunukuu taarifa zao za mafanikio katika utekelezaji wa kilimo hai kwa manufaa ya jamii na wakulima. Pamoja na kuinufaisha jamii kwa mapana, pia ni fursa kwa mkulima aliefikiwa na MkM kujulikana pamoja na kutangaza bidhaa anazozalisha. Katika Makala hii, tutajifunza kupitia mkulima mmoja mkoani Arusha, katika wilaya ya Karatu…