- Kilimo

Mkulima Mbunifu tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya wakulima

Sambaza chapisho hili

Kuna usemi ambao ninaamini kuwa ni wa kweli kabisa, unaosema ufahamu ni njia ya kila jambo unalohitaji kufanya, na taarifa sahihi ni nguvu ya kila jambo. Usemi huu unaweza kudhihirishwa na muda ambao tumekuwa tukichapisha jarida la Mkulima Mbunifu, na kwa namna ambapo wale wote waliolitumia wameshuhudia ni kwa jinsi gani limekuwa msaada mkubwa kwao.

Wafugaji na wakulima walilipokea vizuri sana na tumekuwa tukipata ushirikiano mzuri nchini kote. Kila uchwao tumekuwa tukipokea maombi mapya kutoka sehemu mbalimbali ya wakulima na wafugaji kuweza kupatiwa nakala za jarida hili. Wengine wakiulizia namna ya kupata taarifa fulani, wengine wakiomba tuwatembelee ili waweze kushirikisha wenzao mafanikio yao kupitia jarida hili, na hata wengine wakitupongeza kwa namna ambavyo taarifa hizi zilivyokuwa na manufaa kwao.

Pamoja na hayo yote, tumekuwa tukipokea pia wanaotukosoa kwa nia njema ya kuimarisha na kuboresha matoleo yajayo. Linafurahisha sana kuona kuwa MkM kimekuwa ni chombo muhimu sana kinachowaunganisha na kushirikishana mawazo miongoni mwa jamii ya wakulima nchini Tanzania

Mrejesho ambao tumekuwa tukipokea kutoka kwa wakulima na wadau wengine kuhusiana na yale yanayochapishwa katika jarida hili, ni muunganiko kati ya watafiti, wanasayansi, na mahitaji ya wafugaji na wakulima kuhusiana na shughuli zao, na yale wanayoweza kuyagundua wenyewe, na kuweza kuwanufaisha katika maisha yao ya kila siku.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *