Ni ukweli usiopingika kuwa, wakulima wengi kwasasa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mbolea kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali jambo ambalo huweza kutatuliwa kwa kutumia njia mbalimbali na matumizi sahihi ya mbolea za asili ikiwemo samadi itokanayo na kinyesi cha popo. Popo hupatikana katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye mapagala, miti, mapango au kwa kujenga…
Kilimo
Je, unafahamu kuwa kilimo hai kina kanuni zake za msingi
Kanuni za kilimohai zinavyofungamana na mazingira Kanuni ndio msingi wa kilimo hai na mchango unaoweza kuifanya dunia kuboresha kilimo duniani kwa ujumla. Kilimo ni moja ya shughuli muhimu zinazofanywa na binadamu kwa ajili ya kupata mahitaji ya kila siku ili kujikimu. Historia, mila na tamaduni za watu katika jamii zinaambatana na maendeleo katika kilimo. Kanuni zinazotumika katika kilimo kwa ujumla…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2022
Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…
Je, unafahamu kuwa kilimo hai kinalipa
Bonyeza hapo juu kusikiliza kuhusu kilimo hai
Ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine
Katika toleo lililopita tuliangalia utangulizi wa mada hii ya ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine. Tuliweza kuangazia mambo kadha wa kadha muhimu, na miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na faida za ufugaji huo, pamoja na manufaa ya ufugaji wa namna hiyo; Aina ya samaki wanaofaa katika kilimo mseto Perege na Kambale ni samaki wanaofugwa katika maeneo mabalimbali nchini…
Uzalishaji wa mafuta ya karanga
Karanga hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali au kukaangwa ili kutumika kama vitafunwa lakini pia kusindikwa ili kupata mafuta, siagi na rojo. Karanga zina virutubisho vingi kama vile; maji asilimia 7, nguvu kilokari 570, protini gramu 23, mafuta gramu 45, wanga gramu 20, kalishamu miligramu 49, chuma miligramu 3.8, patasiamu miligramu 680, vitamini B miligramu 15.5 na vitamini A (I.U…
Namna bora ya uhifadhi wa shamba
Shamba ni eneo ambalo mkulima anaweza akalitumia kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji kama vile ufugaji na kilimo kwa lengo la kujipatia chakula na pato. Hata hivyo, baadhi ya wakulima nchini hawana elimu ya kutosha ya namna bora ya kutunz shamba, hivyo kushindwa kuzalisha mazao bora, mengi na yenye tija. Bila shamba hakuna uzalishaji na shamba bila utunzaji hakuna uzalishaji pia…
Ukisoma jarida la Mkulima Mbunifu kila siku utakuwa na tabasamu usoni mwako
Hebu waangalie wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu wakifurahia kupata nakala zao