- Kilimo

Ijue thamani ya mti wa mlonge

Sambaza chapisho hili

Kila sehemu ya mti wa mlonge inathamani na faida nyingi, faida hizo zinaweza kuwa kwa binadamu, wanyama au mimea. Ni jambo jema kwa mkulima yeyote anayefanya au anayetaka kufanya kilimo hai kujifunza namna atakavyo weza kutumia mti wa mlonge na kunufaika na faida zinazotokana na mti huu.

Mti wa mlonge unafaida nyingi ambazo hazifahamiki kwa watu wengi. Faida za mti huu zinatokana na sehemu mbalimbali za kwenye mti wa mlonge ambazo ni maua, majani, magome na matunda. Zina faida nyingi pia kwa afya ya bainadamu. Maua ya mlonge huzalishwa hata kipindi ambacho hakuna mvua, Mti huu unaviinilishe ambavyo huweza kutumika kuboresha afya ya watoto wakati wa njaa.

Majani ya mti huu yanastawi hata kipindi cha ukame ambapo ukuaji wa mazao ya chakula ni mdogo na majani haya yana kiwango kikubwa cha vitamin B na C.

Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimeonyesha kuwa mlonge unafaida zifuatazo:

  • Unaongeza kinga ya mwili
  • Majimaji ya majani yana tumika kama dawa ya ngozi
  • Majimaji ya majani hurekebishwa msukumo wa damu
  • Unapunguza maumivu ya kichwa
  • Maji maji ya majani inatumika kurekebisha kiwango cha sukari mwilini hasa kwa watu wenye tatizo la kisukari
  • Unapunguza uvimbe na maumivu ya viungo
  • Unaongeza kiwango cha maziwa kwa wakina mama wanaonyonyesha
  • Unapunguza maumivu yanayotokana na mafua makali
  • Unapunguza kiwango cha kolesteroli mwilini
  • Mbegu za mlonge hutumika kutengeneza mafuta yenye ubora sawa na mafuta ya alizeti na mzeituni
  • Unaweza kutumika kutengeneza vipoddozi kama sabuni na mafuta
  • Mauwa ya mlonge hutumika kutengeneza chai ya mmea
  • Unga wa majani ya mlonge unapochanganywa na chakula huongeza nguvu mwilini

Mmea wa mlonge ni miongoni mwa mimea ilio na kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye manufaa kwa mwili wa binadamu na mifugo. Unavirutubisho zaidi ya 90 na unaweza kutumiwa na watu wa umri wote. Hakuna madhara yeyote ya kutumia mlonge ambayo yamethibitishwa na wataalamu.

Kiwango cha viinilishe katika mlonge

  1. Mmea wa mlonge una kiwango cha vitamin C mara saba zaidi ya machungwa
  2. Unakiwango cha Vitamini A mara nn zaidi ya karoti
  3. Unakalsiamu maraa 4 zaidi ya maziwa
  4. Unamadini ya chuma mara 3 zaidi ya mchicha
  5. Unamadini ya potasiamu mara 3 zaidi ya ndizi
  6. Majani ya mlonge yana kiwango cha protini mara 2 zaidi ya maziwa

Viini lishe vyenye faida kwa watoto (Mlonge unaitwa “Rafiki kipenzi wa mama”)

Gramu 25 za unga wa majani ya mlonge zinaweza kumpa mtoto mchanga viini lishe vifuatavyo:

  1. Asilimia 42 ya kiwango cha protini kinachoitajika kwa siku
  2. Asilimia 125 ya kiwango cha kalsiamu kinachoitajika kwa siku
  3. Asilimia 61 ya kiwango cha magnesium kinacho hitajika kwa siku
  4. Asilimia 41 ya kiwango cha potasiamu inayohitajika kwa siku
  5. Asilimia 71 ya kiwango cha madini ya chuma kinachohitajika kwa siku
  6. Asilimia 271 ya kiwango cha vitamin A kinacho hitajika kwa siku
  7. Asilimia 22 ya kiwango cha vitamin C kinachohitajika kwa siku

Unapolima mlonge unanafasi kubwa zaidi yakuongeza kipato na kuboresha lishe. Licha ya hivyo Sehemu zote za mmea wa mlonge zina uwezo wa kuongeza kinga ya mwili.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *