Just click here to watch Climate change, biodiversity loss, poverty, health issues: what we eat and how we produce our food is shaping the face of our planet and of our societies like no other human activity. The hidden costs of cheap food are mind-blowing. At the same time, food is currently one of the most powerful levers for changing…
Kilimo
Umuhimu wa wataalamu kwa wakulima na wafugaji
Wataalamu wa kilimo na mifugo wamepata mafunzo ili kuendeleza mbinu za kilimo na mifugo kwa lengo la kutoa faida kwa wakulima na wafugaji. Baadhi ya wataalamu wanaweza kuona upungufu fulani au kuona kuwepo kwa mantiki kwenye baadhi ya mbinu za asili ambazo bado zinatumiwa katika uendeshaji wa kilimo na ufugaji na kuweza kuafikiana na wakulima hao juu ya kuziendeleza au…
Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha kilimo biashara
Mkulima ni mfanyabiashara, na mfanyabiashara yeyote analenga faida kubwa au hasara kidogo sana. Ni muhimu kwa mkulima kujua thamani ya mazao yake ili aweze kujua ni bei gani anayotakiwa kuuzia mazao yake lakini pia ajue bei ambayo akiuza kwayo itamletea hasara. Unapoanzisha mradi wa kilimo biashara, unatarajia mwisho wa siku umalizike kwa kupata faida. Kuna mambo mawili makubwa miongoni mwa…
Kilimo cha kiikolojia kwa wakulima wadogo
Kilimo cha kiikolojia cha wakulima wadogo ni aina ya maisha yanayoichukulia dunia kwa heshima na kuithamini, na siyo kama kitu cha kunyonywa. Ni mfumo wa maisha unaonyesha kuwa upo uhusiano wa karibu kati ya binadamu na mazingira yanayowazunguka na hivyo mazingira hayo yasithaminishwe kwa pesa. Mfumo huu unaoelewa kuwa matumizi mabaya ya mazingira na kuyafanya chanzo cha pesa kutaangamiza watu…
Fursa ya kibiashara kutokana na zao la alizeti
Alizeti ni zao maarufu katika maeneo yenye mvua za wastani mfano Mkoa wa Singida, Dodoma, Manyara na Simiyu. Zao hili limekuwa maarufu sana kutokana na mafuta yake kupendwa na watu wengi kwa sababu hayachanganywi na kemikali yoyote. Katika miaka hii miwili, Mafuta ya alizeti yameonekana kupanda bei kutoka fedha za kitanzania shilingi 3000/= kwa lita hadi 5500/= huku dumu la…
Mkulima avumbua dawa ya asili ya kutibu ugonjwa wa mnyauko
Uzalishaji wa mbogamboga umekuwa maarufu nchini, hasa kutokana na uhitaji wake wa kila siku. Hii ni kutokana na jamii kupata uelewa juu ya umuhimu wa ulaji wa mbogambga kwa afya ya mwili. Aidha, upatikanaji wa soko ndani na nje ya nchi pamoja na uzalishaji kuwa rahisi, umepelekea wakulima wengi kujikita katika kilimo hiki. Hata hivyo, kilimo hiki kimekua na changamoto…
Ewe Mkulima, sikiliza na fahamu changamoto kuu za kilimo hai/kilimo endelevu Africa
Je, wewe ni Mkulima au Mfugaji, Msikilize Mkurugenzi Mtendaji [Biovision Africa Trust] Daktari. David Amudavi akieleza juu ya changamoto kuu za kilimo hai/kilimo endelevu barani Africa. Bonyeza hapa chini kusikiliza https://podcast.ausha.co/voices-for-change/what-are-the-main-challenges-for-organic-and-sustainable-agriculture-in-africa-david-amudavi
Unapouza mazao yako zingatia vipimo sahihi
Wakulima walio wengi wamekuwa wakipoteza mamilioni ya shilingi kutokana na uuzaji wa mazao kwa kutumia vipimo visivyokuwa sahihi Kwa kawaida wakulima wanapoamua kufanya shughuli ya uzalishaji wa mazao huwa na malengo makubwa sana ya kufaidika kutokana na mazao hayo pindi msimu wa mavuno unapofika. Hii imekuwa ni tofauti kabisa kutokana na wakulima kuishia kupata hasara inayosababishwa na kuuza mazao yao…
Sindika karakara kupunguza upotevu
Karakara ni zao la matunda ambalo ni muhimu kwa biashara na chakula linalolimwa katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Kigoma, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha. Mara nyingi wakulima huzalisha zao hili kwa wingi sana kwa msimu mmoja na hatimae kushuka kwa soko lake na kufanya kuwepo kwa upotevu na uharibifu wa matunda haya. Ili kuondokana na uharibifu huu,…
Mkulima Mbunifu yaangazia kilimo hai ZANZIBAR
Kama ilivyo ada, Mkulima Mbunifu hutembelea wakulima wanufaika wa jarida la kilimo hai nchini Tanzania. Hivi karibuni, Mkulima Mbunifu ilitembelea kisiwa cha Zanzibar ambapo iliweza kufanya mahojiano na baadhi ya wakulima wa kilimo hai na wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu Zanzibar. Katika makala hii tutamuangalia Bi. Salma Hussein Makame, Mkulima wa kilimo hai kutoka kijiji cha Unguja Ukuu, Wilaya…