- Kilimo, Mazingira

Panda miti kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi

Sambaza chapisho hili

Wakulima wanaweza kuchangia uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti na kutumia mbinu za kilimo hai. Kupanda miti ina manufaa nyingi ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira, kuwa chanzo cha malisho ya mifugo, asali, mbao, na hewa safi.

Kipindi kirefu cha ukame ambacho kimeripotiwa katika kanda hii ya Afrika Mashariki imesababisha maeneo mengi kuwa kavu na hata ardhi kumomonyolewa na upepo kwa sababu ya kutokuwa na miti, na vichaka kukauka pia. Hali hii imesababisha hali ya hewa katika maeneo mengi ya kanda kutokuwa nzuri, mifugo na binadamu kuteseka na hata kusababisha kipato cha wakulima na wafugaji kuyumba.

Kawaida, baada ya ukame mrefu, matarajio ni kuingia katika msimu wa mvua, ambazo zinategemewa katika maeneo. Sehemu katika kanda ambazo zimepokea mvua kwa viwango vya kawaida zinatarajiwa kuingia msimu wa kiangazi.

Uzalishaji wa chakula unadorora na kusababisha mfumko wa bei wa bidhaa muhimu ya chakula kama vile nafaka, mbogamboga na malisho ya mifugo. Ili kuepuka hali hii ya kuwa na ukame, uharibifu wa mazingira, na hata kuyumba kwa kipato, ni muhimu kujipanga na kupanda miti kuzunguka shamba na mazingira yako.

Hii itasaidia mazingira yako kuwa mazuri hapo baadaye na kukuwezesha kuzalisha kwa utulivu, hali kadhalika kupata hewa safi, pamoja na mifugo yako kupata malisho.

Jambo la kufanya ni kuandaa kiasi kidogo cha fedha, na kwenda kwa wauzaji wa miche ya miti uweze kupata aina ya miti unayohitaji. Pia, unaweza kupanda na kutunza miche yako mwenye shambani mwako. Jambo la muhimu ni kutunza mazingira ili yakutunze.

Anzisha na kutunza kitalu cha miti shambani

Kama kila mkulima atapanda miche mitano ya miti kila mwaka, mashamba yatakuwa na miti ya kutosha kwa siku zijazo, kupunguza uharibifu na upotevu wa misitu michache iliyobaki.

Miti pia imekuwa ni chanzo kizuri cha kipato kwa wakulima, na pia kwa vikundi hasa vya vijana ambao wamejiunga pamoja na kutengeneza vitalu vya miti kwa ajili ya kuuza. Kutengeneza kitalu cha miti kwa ajili ya biashara si ngumu; endapo mkulima ana eneo ndogo kwa ajili ya kitalu hatahitaji kujenga kibanda kwa ajili ya kivuli, kivuli cha

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *