Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…
Kilimo Biashara
Vijana wajiajiri kupitia kilimo hai
Kumekua na muamko wa vijana kutumia fursa ya kilimo kujipatia kipato. Mkulima Mbunifu ilikutana na vijana mkoani Arusha ambao waliamua kujifunza na kutengeneza mboji kwa ajili ya biashara. Kutokana na changamoto za ajira vijana hawa wameweza kubuni mradi na kutumia elimu waliyonayo ya ujenzi wa mitambo ya biogas na utengenezaji wa mbolea hai kama fursa ya kujiingizia kipato. Pia, wanufaikaji…
Namna ya kusindika korosho mara baada ya kuvuna
Korosho ni zao lenye matumizi mengi sana, lakini kubwa kuliko yote ni kwamba kuliwa kama kitafunwa (snacks) wakati wa kunywa chai, juisi, maziwa au kahawa. Makala hii inakusudia kutoa mafunzo ya namna ya kuandaa korosho kwa matumizi ya nyumbani. Hii itawasaidia wakulima wapya wa mikoa hasa iliyoingia kwenye uzalishaji wa zao hili kwa mara ya kwanza. Jinsi ya kuandaa korosho…
Sindika mchicha nafaka kupata bidhaa bora ya unga
Mchicha nafaka ni jamii ya mchicha katika kundi la mboga lakini wenye kulimwa kwa ajili ya kupata nafaka. Mimea yake ni tofauti na mimea ya nafaka nyingine kama vile ngano, mahindi au mtama. Asili ya mchicha nafaka ni huko Mexico, Amerika ya Kusini, na mchicha huu ulikuwa ukitumika kama chakula kikuu cha nchi hiyo ikiwa ni moja ya nafaka. Makundi…
Ukizingatia kanuni sahihi, kilimo cha migomba kina tija
Nchini Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya. Zao la migomba limekuwa muhimu, na kufuatiwa na mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo, viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharagwe. Zao la…
Unaweza kuongezea thamani Mtama kwa kuzalisha mvinyo
“Kwa karne nyingi, mtama umekuwa ukichukuliwa kama chakula cha watu maskini au chakula cha njaa, hili sasa limegeuka na kutoa matumaini mapya kwa wakulima wa mtama nchini Tanzania” Mtama ni kundi la mbegu ndogo ndogo aina ya mazao ya nafaka, yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe. Hii ni aina ya mazao yanayolimwa katika mazingira magumu kama…
Kilimo biashara kina faida kikifanyika kwa njia ya vikundi vya wakulima
Kilimo kitabaki kuwa msingi wa ukuaji wa uchumi kupunguza umaskini na kudumisha mazingira iwapo kitafayika kwa utaratibu. Hata hivyo ni muhimu mkulima kuzingatia kilimo biashara ili kukuza kipato. Kilimo biashara ni fursa muhimu ambayo mkulima anapaswa kufanya kwa kuzingatia utaratibu maalumu. Hii ni pamoja na kufanya tathmini ya biashara ili kuhakikisha kufaulu kwake. Katika makala hii tutaangazia kuhusu kilimo biashara na…
Sindika Mananasi kuzalisha bidhaa mbalimbali
Nanasi huliwa kama tunda na huweza kusindikwa ili kuzuia kuharibika na hivyo kupatikana kwa bidhaa kama jamu, juisi, mananasi makavu na vipande vya mananasi visivyokaushwa.
Namna bora ya uchakataji na uhifadhi wa samaki ili kuzuia wasiharibike
Ufugaji samaki kwa sasa umeshika kasi kutokana na ulaji kuongezeka taktibani katika maeneo yote ya nchi. Ili kuhakikisha kuwa mfugaji anaweza kufanikiwa katika hatua zote za ufugaji mpaka hatua ya kupeleka bidhaa yenye ubora ni muhimu sana kuzingatia uhifadhi. Kwanini uhifadhi wa samaki Samaki kama viumbe vingine visipohifadhiwa vizuri na katika utaratibu maalumu wa kitaalamu, ni rahisi sana kuharibika na…
Unaweza kusindika Nanaa badala ya kuuza majani mabichi
Kabla ya kujifunza namna ya kusindika nanaa (mint), ni vyema tukaangalia kwa ufupi kuhusu zao hili na namna ya kuzalisha. Nanaa ni zao la majani ambalo huzalishwa na kutumiwa kama kiungo. Zao hili la viungo ni muhimu kuoteshwa kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH kuanzia kiwango cha 6 hadi 7. Zao hili huoteshwa kwa kutumia mapandikizi au…