- Kilimo, Kilimo Biashara

Ubunifu wa kilimo hai hushamirisha ujasiriamali

Sambaza chapisho hili

Hivi sasa nchini wakulima wanazalisha matunda na mbogamboga kwa wingi na katika maeneo mengi. Hii ni kwa sababu wanatambua jukumu lao katika kuongeza mapato yao ya kilimo na ustawi wa familia kama lengo la shughuli zao za kilimo. Hivyo ni muhimu wazalishaji kuhakikisha hawakosi mifumo mizuru kwa ajili ya mazao yao.

Ni muhimu wakulima kuhakikisha kunakuwepo na mifumo mizuri ya uzalishaji, uhifadhi, usindikaji na upatikanaji wa taarifa sahihi za masoko ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kukua kiuchumi.

Ni lazima wakulima kubuni mbinu dhabiti za kupunguza gharama ya uzalishaji, kudhibiti magugu, wadudu waharibifu na magonjwa. Baada ya kuzalisha mazao ya hali ya juu, wakulima wanahitaji njia za kuhifadhi mavuno kwa matumizi ya muda mrefu.

Mbali na upatikanaji wa taarifa za masoko kwa wakulima, ni muhimu pia wakulima wakafikiria uwepo wa utaratibu wa inayoeleweka ya kuwafikia wanunuzi ili kujua wanazalisha nini, watapata huduma wapi, watauza wapi, watauza kwa nani na watauza kwa bei gani. Hii itasaidia kuuza bila kudanganywa wala kudidimizwa ili kuendeleza uchumi wao wenyewe.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Ubunifu wa kilimo hai hushamirisha ujasiriamali

  1. Nahitaji mbegu ya kitunguu saumu,Niko Kenya maeneo ya Loitokitok mpakani mwa Kenya na Tanzania

    1. Habari,
      Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuwasiliana nasi. Kuhusu mbegu ya kitunguu saumu, tunakushauri uende sokoni ununue kitunguu saumu kilichokomaa na kukauka vizuri, kisha utumie punje zake ubwa kwa ajili ya kuotesha, usioteshe punje ndogo utapata mavuno hafifu.

      Karibu sana Mkulima Mbunifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *