- Kilimo Biashara

Matumizi mbalimbali ya mlonge

Sambaza chapisho hili

Kusafisha maji

I. Kusanya mbegu za mlonge zilizokomaa kisha zimenye kupata kiini

II. Twanga kiini mpaka upate unga

III. Weka gramu 2 (vijiko viwili vya chai) za unga wa mlonge kwenye maji kiasi (nusu lita) natikisa kwa muda ilikupata mchanganyiko mzuri

IV. Changanya kwenye maji lita 20 na koroga sana kwa muda wa dakika 10-15

V. Yaache maji yatulie kwa msaa 2 juani, utaona uchafu umetuama chini

VI. Yachujie maji kwenye chombo safi na kisha yaweke juani masaa machache. Kwa njia hii kiwango cha madhara ya maji machafu kinapungua kwa asilimia 80-90. Inashuriwa kutumia kiwango cha miligramu 30-300 za unga wa mlonge kwa lita moja ya maji kwa kuzingatia kiwango cha uchafu.

Angalizo: Maji ya chemshwe kabla ya kunywa.

Chakula cha mifugo

Majani mti wa mlonge yanaweza kulisha ngo’mbe, mbuzi, nguruwe, na sungura. Yanaweza pia kutumika kulisha samaki katika mabwawa, Inashauriwa kupanda mlonge karibu na bwawa la samaki.

Mbolea

Mashudu ya mbegu za mlonge yanaweza kutumika kama mbolea zenye kiwango kikubwa cha naitrojeni.

Uzalishaji wa asali

Maua ya mlonge ni mazuri kwa chakula cha nyuki katika uzalishaji wa asali, hivyo inashauriwa kupanda mlonge katika maeneo yenye mazinga ya nyuki.

Kuchanganya na mzao mengine

Kutokana mmea wa mlonge kuwa na mizizi mirefu inayosambaa na hauna kuvuli kikubwa; unaweza kutumika kuchanganya mazao mengine yanayo hitaji kiwango kikubwa cha naitrojeni.

Mbolea ya majani

Maji yanayotokana na majani ya mlonge yanaweza kutumkia kama mbolea ya majani kwani yanauwezo wa kuongeza uzalishaji kwa asilimia 30.

Kutengeneza biogas

Majani ya mlonge yana virutubisho muhimu kwa utengenezaji wa biogas

Mbolea ya kijani

Mlonge ukipandwa kwa wingi kisha ukachanganywa kwenye udongo, unafanya kazi kama mbolea ya saili kwa mazao mengine.

Kuzuia magonjwa ya mimea

Kuchanganya majani ya mlonge kwenye udongo kabla ya kupanda husaidia kuzuia ugonjwa wa kiuno (damping-off) uanao shambulia shina la mmea.

Namna ya kuandaa mlonge kwa matumizi mbalimbali

Majani mabichi ya mlonge

Tumia majani ya mlonge usiokomaa au majani machanga toka mti uliokomaa. Inashuriwa kuongeza majani ya mlonge wakati wa hatua za mwisho wa mapishi ili kutoharibu viinilishe muhimu yaanivitamini na madini.

Unga wa majani ya mlonge

  •  Ili kutengeneza supu ya majani, majani yaliyokaushwa yanaweza kutumika badala ya majani mapichi .
  • Vuna majani ya mlonge toka mtini.
  • Yaoshe kisha yaache yakauke sehemu isiyo na jua (ukianikwa juani virutubisho hupotea).
  • Yatwange majani yaliyokauka ilikupata unga wa longe.
  • Utunze unga wa mlonge kwenye chombo kikavu chenye mfuniko sehemu isiyo na joto.
  • Ongeza vijiko viwili vya mlonge kwenye chakula au mboga ilikuboresha lishe

Maua

  • Maua yana kiwango kiwango kikubwa cha kalsiamu
  • Ni lazima ya chemshwe kabla ya kuliwa

Mbegu

Mbegu za mlonge hutumika kupunguza homa

Zinapoliwa mara kwa mara zinaulinda mwili usipatwe na magonjwa mbalimbali mf. Mbegu nne za mlonge zikiliwa kila siku (mbili asubuhi, mbili jioni) zinasaidia kupunguza maumivi ya viungo na mgogo.

Mafuta ya mbegu za mlonge

Mafuta ya mlonge yanasaidia sana kupunguza maumivu na uvimbe

I. Acha mbegu zikauke zikiwa mtini ndipo uvune

II. Kama hazijakauka zianike juani

III. Ondoa ganda la mbegu ya mlonge kupata kiini

IV. Kamua kama mafuta ya alizeti

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *