Sadick Amri anauliza: Naomba niulize utalijuaje yai lenye uwezo mkubwa wa kutotolewa. Mwang’oko Milamo anajibu: Yai lolote lililotagwa na kuhifadhiwa katika mahala pasafi, bila kushikwa shikwa na mikono yenye mafuta, na kufanya yai lipungue, hutotolewa. Aidha yai lililotagwa na kuku aliyelishwa aliyepata lishe kamili, kuku waliopata ratio nzuri kati yao na majogoo, yai lililotagwa na kuku asiye na matatizo ya…
Kuku wa kienyeji
Ufugaji wa kuku unainua pato la mkulima kwa haraka
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni ndege maarufu na anayefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Kwa nini ni vigumu kuongeza…
Fahamu wadudu wasumbufu katika ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku ni moja ya sekta ambayo imekuwa na faida kwa wafugaji walio wengi, na hata watu ambao wanafanya shughuli nyinginezo, lakini bado hujishughulisha na ufugaji wa kuku. Pamoja na aina hii ya ufugaji kuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea wafugaji kipato kikubwa, bado inakumbwa na changamoto mbalimbali. Mojawapo ya changamoto hizo ni pamoja na uwepo…
Fahamu mikakati rahisi inayoweza kutumika ili kupanua mradi wa ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni ndege maarufu na ana-yefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Kwa nini ni vigumu kuongeza…
Utajuaje kama mayai ya kuku yataanguliwa
Ni jambo jema kufahamu kama mayai yanayoatamiwa na kuku yataanguliwa yote au mangapi hayataanguliwa. Na kwa wanaototolesha vifaranga ni muhimu zaidi kwao kujua hali ya mayai inavyoendelea ndani ya kiangulio na kufahamu kama kuna tatizo linaweza kusababisha kifaranga ndani ya yai kufa. Pia kujua kama kuna mayai ambayo hayatapelekea kutotoa kifaranga na kuyaondoa. Hii yote hufanyika kwa kuyachunguza mayai yanayototolewa…
Ufugaji holela wa kuku haufai na ni hatari
Nimekuwa mfugaji wa kuku kwa kipindi cha miaka mingi sana, tatizo ni kwamba kuku wangu hawana banda maalumu na hukutana nao jioni tu wanapoingia jikoni, na kutoka asubuhi, nimesoma kidogo kwa jirani yangu aliekuwa na Mkulima mbunifu juu ya ufugaji wenye tija, je nikianza haitanigharimu sana kwa kuwa wao hujitafutia chakula wenyewe?-Haule, Iringa. Kuku kama ilivyo kwa mifugo wengine, wanahitaji…
Fahamu sifa, faida na changamoto za ufugaji kuku wa asili
Kuku wa asili ni aina ya kuku ambao wamekuwepo nchini kwa muda wa miaka mingi na damu au koo zao hazikuchanganywa na aina yeyote ya kuku wa kienyeji. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbalimbali. Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa asili nchini Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo wadogo wanaoishi kandokando ya miji na wale wanaoishi hasa vijijini. Kuku hawa…
Wafahamu Nzi Chuma (Black soldier Fly), protini mbadala kwa mifugo
Nzi chuma (Black Soldier Fly), kwa kisayansi Hermetia illucens (Linnaeus) ni aina ya nzi katika kundi la Stratiomyidae ambao hupatikana sana katika ukanda wa Magharaibi mwa hemisphere yaani mabara ya Marekani ya kusini na kaskazini, sehemu ya Africa, Ulaya, Antactical, Asia na pia Australia. Nzi hawa wana protini ya kutosha kulishia mifugo. Nzi hawa hawana madhara ya aina yoyote kwa…
Mikakati rahisi ya kupanua ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima mapato makubwa. Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni mnyama maarufu na anayefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Je, mbona ni ngumu kuongeza…
Chanja kuku kuepuka magonjwa yanayoambatana na mvua
Wafugaji wamekua wakijisahau juu ya umuhimu wa chanjo kwa mifugo, Katika msimu wa mvua za masika, mifugo mingi imekua ikiathirika kutokana na magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bacteria pia virus. Wafugaji wa kuku haswa wakienyeji, wameishia kupoteza mifugo yao kutokana na kutozingatia chanjo. Mara nyingi mvua hizi huambatana na magonjwa mengi kwa kuku kama vile gumboro, ndui ya kuku, kideri, kipindupindu…









