- Mifugo

Unaswali kuhusu ufugaji wa kuku? Wenzako wameuliza na kujibiwa, uliza tutakujibu

Sambaza chapisho hili

Sadick Amri anauliza: Naomba niulize utalijuaje yai lenye uwezo mkubwa wa kutotolewa.

Mwang’oko Milamo anajibu: Yai lolote lililotagwa na kuhifadhiwa katika mahala pasafi, bila kushikwa shikwa na mikono yenye mafuta, na kufanya yai lipungue, hutotolewa. Aidha yai lililotagwa na kuku aliyelishwa aliyepata lishe kamili, kuku waliopata ratio nzuri kati yao na majogoo, yai lililotagwa na kuku asiye na matatizo ya magonjwa, lililotagwa kwenye kiota au kwenye mazingira masafi na yai lilochukuliwa kutoka kwenye kiota kwa wakati hutotolewa iwe na kuku au kwa mashine.

Sadick Amri anauliza: Nauliza vipi kulishika yai kwa mikono litatotolewa? na kulishika ukiwa umepaka majivu kwenye mikono je?

Mwang’oko Milamo: Kuhusu kushika yai kwa mikono iliyopakwa majivu hiyo husaidia kutoa unyevu, harufu au rangi iliyoko mkononi isije ika shika kwanye yai pamoja na kuifanya mikono kuwa mikavu.

Yai likigusa maji baada ya muda uharibika hivyo inashauriwa pia yai la kutotoleshwa lisilowanishwe kwa maji na ikitokea limeshikwa ama kupata maji basi liuzwe au litumiwe kwa ajili ya chakula.

Kwa kupaka majivu mikononi kuondoa harufu husaidia kuku kulalia mayai kwa likiwa na harufu wakati mwingine hufanya kuku kuzila mayai.

 

Sadick Amri anauliza: Naomba niulize majina ya dawa za chanjo ya vifaranga kwa magonjwa ya gumboro, mahepe(mareks), ndui na kideri.

Mwang’oko Milamo anajibu: Majina ya madawa au chanjo hutambulika kwa ugonjwa unaokingwa, hivyo ukihitaji kununua madawa hayo au chanjo hizo utahitajika kutaja jina la ugonjwa unaotaka kuchanja, kwa mfano kwa kideri ni chanjo ya kideri.

Sadick Amri anauliza: Soko la mayai ya kienyeji kwa mkoa wa Dar es Salaam upoje?

mwang’oko milamo: Kwa mara nyingi soko la kuku linalingana ama hukaribiana kwa kiasi kikubwa katika maeneo yote nah ii ni kwasababu kuku wa kuenyeji wanafugwa wachache sana kuliko kuku wa kisasa. Yai moja la kuku wa kienyeji huweza kuuzwa kuanzia shilingi 200 hadi shilingi 500.

Salum Mkwakoa anauliza: Hivi kuku wanaweza kutaga mayai pacha wakati wa kutaga.

Mwang’oko Milamo anajibu: Kuku huweza kutaga yai moja kwa siku. Bali kuna wakati anaweza kutaga yai lenye viini viwili na yai hili halifai kuhatamiwa na kuku kwani huwa ni kubwa kuku atashindwa kuligeuza. Yai hili mara nyingi linashauriwa kutumiwa kama chakula na si kutotolesha.

Sadick Amri anauliza: Ukiwatenga vifaranga na mama yao wale vifaranga utawapatiaje joto?

Mwang’oko Milamo: Mara nyingi kuku hupata joto kwa kuandaa sehemu maalumu ya kuwaweka vifaranga hivyo ikiwa umewatenga na mama yao ni lazima utafute namna ya kuwapatia joto walilokuwa wakipata.

Kwa sababu hiyo, ili uwe na joto zuri ni vema ukatenga eneo dogo la banda kulingana na wingi wa vifaranga na liwe sehemu ambapo hakuna upepo, na ikiwezekana waweza kuzungushia kitu kizito kama blanketi kwenye banda kama ni la mbao ili kuzuia upepo na kuongeza joto bandani.

Kwenye banda, waweza kuweka bulbu za umeme au jiko la la kigae lililo kolea vizuri na lisilokuwa na mwanya wa vifaranga kuweza kupita kwa bahati mbaya na kuunguzwa na moto.

Aidha, ni lazima kuwa makini kwani vifaranga wanaweza pia kufa kwa kuzidiwa na moto au kupungua kwa joto hivyo kama joto ni kali sana huna budi kupunguza kasi ya moto mkaa. Ni vyema zaidi ukatumia chengachenga.

 

Luge Child anauliza: Nimetotolesha vifaranga 50 na nimeweza kuzingatia joto, lishe, usafi, dawa na chumba au banda bora lakini bado wamepatwa na vidonda mdomoni na machon tatizo ni nini?

Mwang’oko Milamo anajibu: Kupata vidonda visivyo na kuumia huweza kuwa ni muendeleza wa dalili za ugonjwa mwingine kwa maana vidonda vya namna hiyo haviji kwa siku moja.

Ni muhimu kujua kama kulikuwa na dalili za awali ambazo yawezekana hukuzitambua mapema mfano mafua’ machozi, uchafu kwenye macho ndizo zilizopelekea kupata vidonda hivyo.

Mara nyingi,  matatizo ya macho kuvimba yanatokana na ugonjwa wa macho ama mafua hivyo ni muhimu kupeleka kifaranga kimoja maabara ili kupimwa au kumuona daktari wa mifugo aliye karibu na wewe ili aweze kuchunguza vifaranga hao. Visababishi vingine pia yaweza kuwa ni mabadiliko ya hali yahewa ama uchafu.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *