Swali: Endapo nitachanja kuku wangu dhidi ya mdondo lakini jirani zangu hawakuchanja kuku wao, je kuku wangu hawataathirika na ugonjwa unapotokea kwa majirani? Jibu: Kinga itokanayo na chanjo hufikia kiwango cha juu kabisa siku ya 14 na endapo ugonjwa utafika kwa jirani yako wakati kuku wako wamekwisha fikia kiwango kizuri cha kinga basi ni dhahiri kwamba hawataathirika kwa ugonjwa huo.…
Kuku wa kienyeji
Mfugaji mashuhuri wa kuku wa kienyeji Singida
Kama ilivyo ada, Mkulima Mbunifu tumekuwa tukikufikishia taarifa toka kwa wakulima katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanaojishughulisha na kilimo ikolojia nia yetu ikiwa ni kuwawezesha wakulima wengine kujionea na kujifunza ni kwa namna gani wakulima wenzao wameweza kufanikiwa katika kilimo ikolojia. Miongoni mwa wakulima waliopata fursa ya kutembelewa na kuhojiwa na jarida hili ni mfugaji toka mkoani Singida ambaye anajishughulisha…
Mchanganyiko sahihi wa lishe/chakula cha kuku kwa kuzingatia gharama nafuu
Hili ni swali alilouliza mkulima Nelson Shao. Habari Nelson , Karibu sana Mkulima Mbunifu na hongera kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za Mkulima Mbunifu. Kuhusu chakula cha kuku unaweza kutengeneza mwenye kama ifuatavyo; Malighafi aina ya kwanza na kiwango Mahindi kilogramu 40 Pumba ya mahindi kilogramu 25, Mtama kilogramu 5 Mashudu ya alizeti kilogramu 10 Dagaa kilogramu 4…
Namna ya kufanya candling (uchunguzi wa mayai yanayototoleshwa)
Makala hii ni muendelezo wa makala iliyopita ambapo ilijikita katika kuelezea namna ya kutotolesha mayai kwa njia ya asili na pia kwa njia ya mashine (Incubator). Katika muendelezo huu tutaangalia kwa undani jinsi ya kuchunguza yai kwa kutumia mwanga. Candling ni njia ya kuchunguza mayai kwa kutumia mwanga aidha wa mshumaa au tochi. Tochi ambayo ni kifaa cha kisasa ni…
MAYAI YANAWEZA KUHIFADHIWA KWA MUDA MREFU BILA KUHARIBIKA
Wakulima wanaowekeza kwenye mradi wa kuku, hupata hasara pale ambapo hawatunzi mayai ipasavyo. Mayai ni bidhaa hafifu na inayoharibika kwa haraka, hivyo, ni lazima ishikwe kwa uangalifu na kutunzwa vizuri baada ya kutagwa ili yasivunjike au kuharibika. Watu wengi wanaonunua mayai kutoka dukani watatambua mara moja kuwa mayai hayo yamevunjika au yameoza. Tatizo hili linaweza kutokana na utunzaji na uhifadhi…
Mikakati ya kupambana na magonjwa ya kuku ili kupunguza hasara
Magonjwa ya kuku huweza kukatiza uzalishaji kwa muda mfupi sana. Mfugaji anafaa kujenga uelewa na uzoefu wake katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya kuku. Cha muhimu ni kuweka mikakati ya kuzuia na yanapotoka mfugaji achukuwe hatua za haraka ili kupunguza madhara. Kuku ni mnyama anayefugwa kwa wingi. Karibu kila kaya lina kuku wanaofugwa kwa ajili ya chakula, hii ikiwa ni…
Kuroila: Kuku wa ajabu wenye faida kubwa
Kuroila wanaweza kufugwa ndani na kulishwa katika banda au kuachiwa huru kujitafutia. Wanaweza kulishwa kwa kutumia mabaki ya vyakula au vyakula maalumu. Kuroila ni aina ya kuku wa kienyeji ambao wanakuwa kwa haraka sana na hutaga mayai mengi zaidi ukilinganisha na aina nyingine ya kuku, wawe wa kienyeji au wa kisasa. Kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki, kuku…
Ni muhimu kuzingatia ubora wa chakula cha kuku kabla ya kununua na kulisha
Ili kuku waweze kuishi, kukua na kuleta matokeo chanya ni lazima wale chakula kingi chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa chakula cha kuku ni lazima uzingatie makundi ya chakula ambazo ni, vyakula vya kutia nguvu, kujenga mwili, kuimarisha mifupa, kulinda mwili pamoja na maji. Vyakula vya kutia nguvu Vyakula vya kutia nguvu vinaweza kuwekwa katika makundi matatu; Kundi la…
Jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe
Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa. Chakula cha kuku ni lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko ufuatao: Vyakula vya kujenga mwili kama vile…
Je, unawatendea haki kuku wako kulinda afya zao na yako
Kumekuwa na imani potofu kutoka kwa watu wengi ikiwamo mafunzo ya kigeni kuwa ufugaji wa kuku kwenye vibanda vidogo vya chuma visivyowapa nafasi ya kutoka ndiyo ufugaji wa kisasa wenye tija jambo hili ni hatari na ukiukwaji wa haki za wanyama. Kuku ni aina ya ndege wanaofugwa na binadamu kwa madhumuni mbalimbali. Asili ya ndege hawa kama ilivyo kwa wengine…









