Majani ya malisho ya umuhimu mkubwa kwa mfugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo. Bila malisho ya kutosha mfugaji atagaramika kwa kununua nyasi hasa wakati wa kiangazi. Kuwa na malisho ya kutosha inampa mkulima amani na hakikisho kwamba mifugo wake wanapata lishe ya kutosha nyakati zote. Ikiwa mfugaji hataweka mikakati ya kuzalisha na kuhifadhi malisho basi mifugo hawatakuwa wenye afya na…
Mifugo
Je, unayafahamu haya kwenye ufugaji wa Samaki?
Wakulima wengi hasa wanaotumia maji ya bomba wangependa kuanza ufugaji wa samaki lakini huenda kuna mambo kadha wa kadha hawafahamu kuhusu ufugaji kwa kutumia maji ya bomba. Aidha, mambo ni mengi ya kuzingatia ili kuanza ufugaji wa samaki lakini tuanze kujibu maswali haya kutoka kwa mkulima anayetaka kufanya ufugaji huu. Husein Mshegia anauliza: Natarajia kufuga samaki kwa kutumia maji ya…
Mkulima Mbunifu imeniongezea maarifa katika ufugaji wa kuku
Rose Rafael Mollel (35) nina Watoto wanne. Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji. Nilianza na kuku 10 tu ambao walinipa changamoto kuwafuga kwani kuku watatu walikufa kwa ugonjwa wa kideri. Nikajiuliza nitafanyaje sasa na sipendi kutumia madawa ya kemikali! Nikabuni chanjo ya kienyeji: tangawizi nikaisaga, matone ya myaa na chumvi kidogo nikakoroga nikawapa vijiko vitatu asubuhi na vitatu jioni.…
Ugonjwa wa Ormilo
UNAFAHAMU KUHUSU UGONJWA HUU! USIACHE KUSOMA JARIDA LA MKULIMA MBUNIFU TOLEO LIJALO LA APRILI!
Vyanzo vya virutubisho
Ni vyema kujenga uelewa wa vyanzo vya virutubisho vinavyoweza kutumika katika kilimo hai. Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo. Kuna mwingiliano kati ya uzalishaji wa mimea na mifugo na unachangia katika kurutubisha udongo. Mabaki ya mazao hulisha wanyama na samadi ya wanyama hurutubisha udongo. Pia, mifugo hao, kama madume, wanaweza…
Busta ya asili
Busta za asili ni nyongeza ya virutubisho kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa mmea ili kua na uzalishaji mzuri hususani pale ambapo mimea imeanza kuzorota kutokana na kupungua/kukosekana kwa virutubisho vya kutosha kwenye udongo, busta hizi zina sifa ya kuupa mmea virutubisho kwa haraka sana na kuleta matokeo mazuri kwenye mimea ndani ya muda mfupi(siku 3). Aina za busta 1.…
Ufugaji wa ng,ombe wenye tija
Naomba ushauri, nina ng’ombe mmoja ambaye namfuga ndani. Amezaa uzao wa kwanza ndama dume. Kwa sasa, ninapata lita 10 kwa siku. Ng’ombe ana uzito wa kilo 400. Gharama za utunzaji ni 70%. Nifanye nini ili awe na tija? Faida zinazotokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa zinatokana na kujumuisha mambo mawili muhimu; aina ya ng’ombe na utunzaji wake. Utunzaji huchukua…
Mkulima hupaswi kuwa maskini
Swali hili limekuwa likijirudia mara kwa mara, kuwa ni kwa nini wakulima wawe maskini? Kwa watu walio wengi hata wakulima wenyewe, wana majibu mengi sana ambayo wamekuwa wakiyatoa, hasa katika kutetea huko hiyo, huku wakiweka kuwa wao ni watu wa chini na wanaokubaliana na hali hiyo ya umaskini. Kuna wale ambao watasema kuwa ni maskini kwa sababu ya zana duni…
Namna ya kufanya candling (uchunguzi wa mayai yanayototoleshwa)
Makala hii ni muendelezo wa makala iliyopita ambapo ilijikita katika kuelezea namna ya kutotolesha mayai kwa njia ya asili na pia kwa njia ya mashine (Incubator). Katika muendelezo huu tutaangalia kwa undani jinsi ya kuchunguza yai kwa kutumia mwanga. Candling ni njia ya kuchunguza mayai kwa kutumia mwanga aidha wa mshumaa au tochi. Tochi ambayo ni kifaa cha kisasa ni…