Mifugo

- Mifugo

Fahamu wadudu wasumbufu katika ufugaji wa kuku

Ufugaji wa kuku ni moja ya sekta ambayo imekuwa na faida kwa wafugaji walio wengi, na hata watu ambao wanafanya shughuli nyinginezo, lakini bado hujishughulisha na ufugaji wa kuku. Pamoja na aina hii ya ufugaji kuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea wafugaji kipato kikubwa, bado inakumbwa na changamoto mbalimbali.  Mojawapo ya changamoto hizo ni pamoja na uwepo…

Soma Zaidi

- Mifugo

Ugonjwa wa ng’ombe wa mapele ngozi

Ugonjwa wa mepele ngozi, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kisayansi kwa jina la Capri poxvirus. Takribani asilimia 5 hadi 50 ya ng’ombe katika kundi wanaweza kupatwa na ugonjwa huu, ambapo ng’ombe wa umri wowote anaweza kupatwa na ugonjwa huu. Ugonjwa wa mapele ngozi hauambukizwi kwa binadamu. Chanzo cha maambukizi na namna ugonjwa unavyoenea Maji maji yanayotoka kwenye vidonda na…

Soma Zaidi

- Mifugo

Tuelimishane kuhusu mradi wa samaki kwa uzalishaji wenye tija

Ni mazingira gani yanafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki! Emma Peter anauliza: Nimefuatilia sana huu ujasiriamali kweli nimevutiwa na ningependa kujaribu kufanya. Nina eneo Rukwa lenye maji yakutosha ya asili takribani mita za mraba 2000, naomba ushauri wako Musa, Jinsi ya kuandaa hayo mabwawa na wapi nitapata samaki hasa sato maeneo ya Mbeya au karibu na Rukwa. Musa Said anajibu:…

Soma Zaidi

- Mifugo

Karibu maonyesho ya Nane Nane 2020

Kama ilivyo ada kila mwaka nchini Tanzania, wakulima hujumuika pamoja kusherehekea wiki ya kitaifa ya kilimo ambayo hufanyika kikanda nchini Tanzania. Maonyesho hayo mahususi hutoa fursa kwa wakulima kufahamiana na kuonesha bunifu mbalimbali, nyenzo za kilimo, usindikaji na masoko ya bidhaa mbalimbali za kilimo. Mwaka huu maonyesho hayo yatafanyika kitaifa mkoani Simiyu, Mkulima Mbunifu itashiriki kikamilifu hivyo usiache kututembelea katika…

Soma Zaidi

- Mifugo

Fahamu na dhibiti ugonjwa wa Coenurosis

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na viluwiluwi vinavyojulikana kitaalamu kwa jina la Coenurusis Cerebralis unaoshambulia mfumo wa fahamu wa kati (ubongo na uti wa mgongo) wa mbuzi na kondoo.                     Chanzo cha viluwiluwi Viluwiluwi vya ugonjwa huu vinatokana na minyoo aina ya tiniamaltisepts iliyopo katika utumbo wa mbwa au wanyama pori jamii…

Soma Zaidi

- Mifugo

Zalisha bilinganya nyeupe kuongeza pato na lishe

Bilinganya nyeupe (Long White Eggplant) ni moja ya zao la mbogamboga ambalo lina viini lishe vingi na muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, Vitamini A, B na C, wanga, protini na maji. Kisayansi zao hili hujulikana kama Solanum Melongenai na kilimo chake huweza kufanyika katika majira yote ya mwaka. Hali ya Hewa Zao hili huhitaji hali ya…

Soma Zaidi

- Mifugo

Jifunze namna ya kuhifadhi mazao ya mikunde baada ya mavuno

Kabla mkulima hajavuna mazao yake, ni vyema akatambua namna ya kuyahifadhi kwa lengo la kuhakikisha zao linabaki katika ubora wake kwa muda mrefu. Kwa nini kuhifadhi Mazao yanapovunwa, ni vyema kuhifadhiwa ili kuhakikisha usalama wa chakula katika kaya na taifa kwa ujumla. Kuweka akiba kwa matumizi ya baadaye au kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya mbegu. Mikunde huhifadhiwa kwenye maghala…

Soma Zaidi

- Mifugo

Ubora wa zizi huinua uzalishaji wa mbuzi na kondoo

Ufugaji wa Mbuzi na kondoo ni wa gharama nafuu sana hasa ukilinganisha na ng’ombe kwani wanyama hawa wana uwezo wa kuishi mahali popote na katika mazingira magumu kama yenye maradhi na ukame. Wanyama hawa kulingana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo huku wakihudumiwa na familia zenye nguvu kazi ndogo na kipato cha chini. Wanyama hawa ambao hufugwa…

Soma Zaidi