Almonds au lozi ni jamii ya karanga zinazovunwa kutoka katika miti mikubwa kama ya mikorosho na karanga hizi ni lishe ambayo inaweza kutumika kwa kupikia au kula kama zilivyo. Asilimia thelathini ya lozi duniani hupandwa huko Califonia kutokana na kupenda hali ya hewa ya Mediterranean. Aidha, huliwa zaidi maeneo ya kusini mwa Ulaya, Kaskazini mwa Afrika, na baadhi ya nchi…
Mifugo
Je, unafahamu sababu za kuku kutaga mayai madogo!
Jarida hili limekuwa mstari wa mbele katika kukudondolea mada mbalimbali zenye tija katika nyanja za ufugaji na kilimo. Mara nyingi mada hizo hujikita katika njia zinazotumika kuzalisha kiasili. Katika toleo hili tutakudondolea moja wapo ya changamoto zinazowakabili wafugaji wa kuku na namna ya kuondokana na changamoto hizo. Zifuatazo ni sababu au hali inayowakumba kuku na kusababisha kuku kutaga mayai yanayoonekana…
Wafahamu Nzi chuma (Black soldier Fly), protini mbadala ya mifugo
Nzi chuma (Black Soldier Fly), kwa kisayansi Hermetia illucens (Linnaeus) ni aina ya nzi katika kundi la Stratiomyidae ambao hupatikana sana katika ukanda wa Magharaibi mwa hemisphere yaani mabara ya Marekani ya kusini na kaskazini, sehemu ya Africa, Ulaya, Antactical, Asia na pia Australia. Nzi hawa hawana madhara ya aina yoyote kwa binadamu kwa sababu hawana mfumo wa chakula mwilini…
Fahamu na uzingatie kanuni bora za ufugaji wa mbuzi na kondoo
Uchaguzi wa Mbuzi/Kondoo wa Kufuga Madhumuni ya kuchagua mbuzi au kondoo wa kufuga ni kuboresha uzalishaji na kuendeleza kizazi bora. Kuna aina nyingi za mbuzi/kondoo wanaoweza kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji. Uchaguzi hufanyika kwa kuangalia umbile, uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa, ukuaji wa haraka, uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi. Mbuzi/kondoo…
Ni muhimu kutambua minyoo inayoshambulia mazao
Mara nyingi tumekuwa tukizungumza kuhusu wadudu rafiki na halikadhalika kuweka wazi kuhusu wadudu wanaoshambulia mazao. Katika toleo hili tutajifunza kuhusu minyoo inayoshambulia mazao. Ipo minyoo ya aina nyingi ambayo inafaida katika urutubishaji wa udongo na mingine ambayo ina madhara kwa mimea, wanyama pamoja na binadamu. Minyoo hutofautiana kwa ukubwa wa maumbile, mfano ipo inayoonekana kwa macho ya kawaida na ile…
Je, tunajali lishe bora kwa ajili ya watoto wetu kila siku?
Tofauti na ilivyo kwa watu wazima, watoto wanahitaji kupata lishe bora kila siku ili kuweza kujenga miili yao, na kukua katika kiwango kinachotakiwa na hatimae kuwa watu wazima. Ni muhimu kufahamu lishe inayotakiwa kwa watoto. Lishe bora ni nini? Lishe bora ni mlo unaojumuisha uwiano unaotakiwa wa virutubisho vyote muhimu vinavyotakiwa kutoka katika makundi makubwa ya vyakula. Miili yetu huhitaji…
Usimamizi wa rutuba ya udongo kwa njia za kilimo hai
Usimamizi wa rutuba ya udongo sio tu kuweka mbolea au kupata mavuno mengi peke yake. Ni kuhusu kujenga udongo wenye rutuba thabiti na hai. Mifumo ya kilimo yenye uzalishaji endelevu inahitaji usimamizi mzuri wa rutuba ya udongo ili kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa uzalishaji wa chakula wa kwao wenyewe. Ndio sababu kwa nini usimamizi sahihi wa rutuba ya…
Soko na utayarishaji wa mazao ya nguruwe
Kwa muda mrefu na katika makala tofauti, MkM imeeleza kwa undani namna nzuri ya uzalishaji wa nguruwe bora, pamoja na lishe yake na mambo kadha wa kadha yanayohusiana na nguruwe. Katika makala hii utapata kufahamu kuhusiana na soko na namna ya utayarishaji wa mazao. Soko la mazao yatokanayo na nguruwe ni sawa na soko la mazao mengine yaliyo sokoni na…
Nimepata mafanikio makubwa katika utengenezaji na matumizi ya mbolea ya maji
Mkulima anaweza kupunguza gharama, kuongeza rutuba kwenye udongo, mavuno pamoja na kipato kwa kutengeneza mbolea mwenyewe. Mimea inaweza kukuonyesha inahitaji nini. Ni rahisi sana kugundua endapo mimea haipati virutubisho vya kutosha. Majani kubadili rangi ni ishara tosha kuwa mimea ina upungufu wa virutubisho. Ni lazima mkulima awe tayari kutatua tatizo hilo kwa haraka kabla hali haijawa mbaya. Upungufu wa madini…
Jinsi ya kugundua upungufu wa virutubisho katika mmea
Nitrogen Dalili: Mahindi, maharage na mboga hukua kwa taabu sana, majani yanakuwa na kijani mpauko. Sukumawiki na kabichi majani yanakuwa na mchanganyiko wa rangi ya njano. Majani ya chini ndiyo huathiriwa kwanza, na kiwango cha maua kuchanua hupungua au kuchelewa. Kutibu: Ongeza kiasi cha kutosha cha mbolea za asili. Panda mimea inayosaidia kuongeza nitrojen kama lablab, desmodium(figiri) na lusina. Weka…






