- Mifugo

Fahamu kuhusu karanga lozi na faida zake kiafya

Sambaza chapisho hili

Almonds au lozi ni jamii ya karanga zinazovunwa kutoka katika miti mikubwa kama ya mikorosho na karanga hizi ni lishe ambayo inaweza kutumika kwa kupikia au kula kama zilivyo. Asilimia thelathini ya lozi duniani hupandwa huko Califonia kutokana na kupenda hali ya hewa ya Mediterranean. Aidha, huliwa zaidi maeneo ya kusini mwa Ulaya, Kaskazini mwa Afrika, na baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati.

Almond ina virutubisho vingi na ni chanzo kizuri cha fiber, protini na mafuta mazuri. Pia, ni chanzo bora cha vitamini E, manganese, na magnesiamu.

Matumizi ya lozi

Almond zinaweza kuliwa kama vitafunwa au kuongezwa kwenye chakula. Aidha, bidhaa zinazotokana na almond unazoweza kuzitumia ni pamoja na maziwa na sagi.

Karanga za lozi

Karanga hizi huvunwa kutoka kwenye matunda ya mti uitwao Prunus dulcis maarufu kama mti wa almonds. Ni karanga nzuri kutumia kwa sababu ya kiwango chake kidogo cha wanga.

Faida za karanga za lozi

  • Zina kiwango kidogo cha wanga hivyo inafanya zitumike kwa uhuru kwa wagonjwa wenye kisukari, presha, uzito mkubwa, kitambi, pumu, ugumba na yeyote anayetaka Kupunguza matumizi ya wanga na sukari
  • Unga wa karanga za almondi unaweza kuutumia kutengeneza mikate, keki, mandazi kwa wagonjwa wote wanaoteseka na magonjwa ya lishe, hutumika mbadala wa ngano
  • Unapozitumia haziwezi kukuletea gesi yoyote, Unaweza kula jinsi zilivyo,Unaweza kuzisaga ukatengeneza kitafunywa upendacho na humeng’enywa vizuri kwenye mfumo wa chakula hila kukuletea gesi
  • Zina kiwango kingi cha mafuta mazuri yaani Omega 3, husaidia kutibu majeraha ya mwili, kulainisha mishipa ya damu na kutibu majeraha yake, Na husaidia sana mtu mwenye magonjwa ya mashambulizi ya mwili kama pumu, baridi yabisi, presha, pumu ya ngozi nk.
  • Hukata njaa haraka sana kwa sababu ya kiwango chake kingi cha protini, Hivyo kukufanya umudu kukaa muda mrefu bila kula chochote bila kujishinikiza na mwili unakuwa unajitibia kwa kiwango kikubwa wakati huo.
  • Zina kiwango kingi cha magnesium na manganese ambacho husaidia kuendesha zaidi ya shughuli za mwili 300 na husaidia kukufanikishia matunda haraka kiafya kama unaumwa.
  • Ina kiwango kingi cha Vitamin E ambacho hukusanya sumu zote mwilini yaani Free radicals ambazo husababisha magonjwa kama pumu presha maumivu ya hedhi, baridi yabisi, kipanda uso, nk.
  • Zimeonesha uwezo mkubwa wa Kurudisha afya ya mwili kwa wanaoteswa na kisukari, presha, pumu ndani ya muda mfupi endapo akitekeleza pamoja na sayansi ya mapishi.
  • Kiwango kingi cha magnesium ndani yake, hupatia mwili na kuwezesha mishipa ya damu kusukuma damu vizuri na kwa ufanisi mkubwa. Kwani unapopungukiwa magnesium unaweza kupata presha hata kama huna kitambi, wala uzito mkubwa.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

6 maoni juu ya “Fahamu kuhusu karanga lozi na faida zake kiafya

  1. Hellow,

    Nimefurahishwa sana na makala yenu hasa hii ya Karanga Lozi, nilichokua nataka kufahamu zaidi ni kwa namna gani nitapata mbegu au miche ya mimea hii na niko Morogoro je inastawi?

    1. Tunashukuru sana kwa kuendelea kuwa mdau wetu wa jarida la Mkulim Mbunifu, kwasasa hatuna uhakika wa mahali pa kupatia mbegu wala miche lakini tutalifanyia kazi na tukipata uhakika wa upatikanaji tutakupa taarifa.

    2. Nahitaji Nijue Bei Yake Na Upatikanaji Wa Hizo Karanga Lozi Mimi Nipo Dares salaam

      1. Habari Bw. Gordon
        Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za Mkulima Mbunifu. Kama upo Dar, ni rahisi sana kuzipata japo bei zipo tofauti tofauti kulingana na kiasi, yaani unaweza kupata kuanzia 15,000/= kwa gramu 500 na zinapatikana kwenye supermarket/au maduka makubwa.

    1. Habari,

      Tunashukuru sana kwa swali lako. Hatuna hakikika kama zinaweza kustawi au la, lakini unaweza kuotesha kidogo kujaribu.

      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *