Wakulima na wafugaji wanashauriwa kuwa katika vikundi au vyama vya ushirika ili kukuza na kupanua kilimo biashara. Ushirika ni biashara zinazojikita kwa watu; zinamilikiwa, zinadhibitiwa na zinaendeshwa na wanachama na kwa madhumuni ya kufikia mahitaji na malengo yao ya pamoja, ya kiuchumi, kijamii, na kitamaduni. Kupitia vyama vya ushirika, wakulima wanaweza kuokoa pesa kutokana na gharama za usafiririshaji wa maziwa…
Mifugo
Siku ya tokomeza gugu karoti Arusha (2020)
Athari za gugu karoti na mbinu za kukabiliana nalo Gugu karoti ambalo kitaalamu linajulikana kama (Parthenium hysterophorus) ni mmea vamizi ambao una athiri binadamu, mazao, wanyama au mifugo pamoja na kuharibu uoto wa asili. Nchini Tanzania, gugu karoti limegundulika au kuonekana kuwepo tangu mwaka 2010 katika mkoa wa Arusha hasa maeneo ya pembezoni mwa baadhi ya barabara, na baadaye kuanza…
Nini husababisha magonjwa kwa mifugo
Magonjwa mengi ya mifugo husambazwa na vijidudu ambao huingia kwenye mfumo wa damu na kusababisha homa na baadae madhara makubwa. Mangonjwa mengi ya mifugo husababishwa na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano mazingira machafu anayoishi mnyama, vitu vinavyosababisha vidonda na ambazo vimelea vinaweza kukaa. Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana na hali za ndani ya mwili kama upungufu…
Zikaushe mboga za ziada kwa matumizi ya baadaye
Kukausha mavuno kutoka shambani mwako, ni njia nzuri zaidi kukuwezesha kukabiliana na hali ngumu. Kukausha mboga na matunda ni njia rahisi sana ya uhifadhi inayotumika duniani kote. Hata hivyo, ili kupata matokeo mazuri na bora, baadhi ya kanuni ni lazima zifuatwe. Kukausha kwa jua Jua hutumika kwa mazao ambayo hayaharibiki yanapokaushwa kwa kutumia jua moja kwa moja, mfano maharagwe, karanga…
Vuna zaidi kwa kutumia mbinu ya tumbukiza
Tumbukiza ni mbinu inayofaa katika eneo ambalo ni kame na lisilokuwa kame. Ni mbinu ya kuhifadhi maji, na kutoa mavuno mengi zaidi. Ni mbinu ambayo imepokelewa kwa kiasi kikubwa na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka sehemu ambazo wana eneo dogo kwa ajili ya uzalishaji wa malisho. Ni ufumbuzi ambao umeonekana kuleta ongezeko la uzalishaji wa matete kwa asilimia 20…
Hifadhi Guatemala kwa malisho wakati wa kiangazi
Majani haya yanatumika kama chakula cha ziada kwa mifugo wakati wa kiangazi, hayatakiwi kutumika kama chakula kamili. Majani aina ya Guatemala (Tripsacum andersonii) imesambaa kwa kiasi kikubwa katika ukanda wa tropiki. Aina hii ya majani inahitaji kiasi kikubwa cha mvua, au udongo wenye unyevu, lakini hata hivyo huweza kubaki yakiwa na kijani kibichi wakati wote wa kipindi cha kiangazi. Nchini…
Umuhimu wa wakulima kuwa kwenye vikundi
Mimi ni msomaji na mdau wa jarida la Mkulima Mbunifu, ingawa sina kikundi. Napenda kufahamu kuwa ni kwa nini mmekuwa mkisisitiza wakulima kuwe kwenye vikundi, na ndipo wapatiwe huduma za Mkulima Mbunifu, nini umuhimu wa kuwa kwenye kikundi? Kikundi ni muunganiko wa watu wenye nia/lengo moja katika kutekeleza jambo fulani walilolikusudia kwa faida ya hao walioamua kuwa pamoja. Lengo kuu…
Ulaji wa bamia na faida zake mwilini
Moja ya zao lenye faida mwilini ni bamia kama tunda mboga kwani linaweza kukutoa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa sababu ya uwezo wake wa kusaidia kuyeyusha au kumeng’enya sukari na kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini. Mara nyingi tumekuwa tukichukulia bamia kama mboga ya kimasikini pasipo kujua kuwa bamia ni tunda mboga lenye faida nyingi sana mwilini…
Boresha kundi lako la kondoo kwa kuzalisha chotara
Njia ya haraka zaidi ya kuboresha kundi lako ni kuzalisha kondoo chotara. Inashauriwa utumie kondoo wa kienyeji kama wanyama wa kuanzia mpango wa kuzalisha kondo bora zaidi. Unaweza kutumia kondoo jike wa kienyeji aina ya Red Maasai na dume wa kigeni aina ya Dorper. Kondoo wanaozaliwa watabeba sifa za aina hizi mbili za kondoo (Red Maasai na Dorper). Njia hii…
Hifadhi vyakula kuepuka njaa wakati wa ukame
Hifadhi mazao ili uweze kuwa na chakula kwa muda mrefu bila kuharibika. Utunzaji pia husababisha vibaki na ubora pamoja na kurahisisha upatikanaji muda mwingi kwa ajili ya chakula. Mara nyingi wakulima hupambana shambani kwa ajili ya kuzalisha chakula ambacho pasi na shaka ndio hulisha watu wote waliopo vijijini na mijini. Pamoja na kujishughulisha huko hujikuta wanabaki bila akiba ya chakula…