Loseriani Sikayoni: “Nimepungunza ujinga kwa kiasi kikubwa baada ya kusoma jarida la Mkulima Mbunifu. Nimejua namna ya kufanya kilimo cha mzunguko, natunza mifugo yangu kisasa, faida ni kubwa.” Ndivyo alivyoanza kusema mzee Loseriani Sikayoni mkulima kutoka kijiji cha Ilkiding’a, mkoa wa Arusha. Kwa miaka mingi, mzee huyu amekuwa akifanya shughuli za kilimo, na maisha yake kwenda vizuri; ikiwa ni pamoja…
Kilimo
Maji moto (weaver’s ant) wadudu rafiki wanaowezesha kilimo hai
Maji Moto au Sangara ni aina ya wadudu, ambao ni rafiki kwa mkulima yeyote anayefanya shughuli zake kwa kuzingatia misingi ya kilimo hai. Ni wadudu wadogo sana ambao huishi katika miti ya mikorosho pamoja na miembe. Mara nyingine hupatikana pia katika pamba. Ikumbukwe kuwa tangu kuumbwa dunia, kila kitu kilikuwa kiasili, watu walikula vyakula na matunda ambayo yalikuwa katika mfumo…
Samadi ya wanyama na mimea
Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni. Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho. Samadi iliyo tayari kwa matumizi Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa…
Mapapai bora hupelekea soko lenye tija
Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamin A na madini ya kalsiamu kwa wingi na zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini kwa wastani wa tani 2,582 kwa mwaka. Ili kuweza kuzalisha zao la papai kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa ni muhimu kuhakikisha unazingatia kanuni zote za kilimo bora za uzalishaji wa mapapai. Ubora…
Jifunze namna bora ya ubebeshaji wa miche ya matunda mbalimbali
Ubebeshaji maana yake ni uunganishaji wa sehemu mbili au zaidi za mimea tofauti na kuwa mmea wenye shina moja. Ubebeshaji hufanyika katika mimea ya mazao ambayo yako katika jamii au ukoo mmoja kwa mfano; embe dodo na viringe, chungwa na limao, parachichi aina ya hass na la kienyeji, passion zambarau na njano, biringanya za aina tofauti, maua ya waridi ya…