Mahindi ni zao la kwanza katika mazao makuu ya nafaka hapa nchini. Huzalishwa kwa wastani wa tani 2393000 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 63 ya mazao yote ya nafaka nchini. Zao la mahindi hulimwa karibu katika mikoa yote, lakini hulimwa zaidi katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Mwanza na Shinyanga. Licha…
Kilimo
Ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine
Katika ufugaji mseto wa samaki na mazao mengine mambo kadha wa kadha ni muhimu sana kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kujua aina ya samaki wanaofaa kufugwa, faida za mboga na hata mifugo mingine kama kuku wanaojumuishwa katika ufugaji huu. Aina ya samaki wanaofaa katika kilimo mseto Perege na Kambale ni samaki wanaofugwa katika maeneo mabalimbali nchini Tanzania. Perege ndiyo aina…
Kutibu udongo kwa kutumia njia ya mvuke au mionzi ya jua
Katika toleo lililopita, tuliangazia kwa undani kidogo kuhusu njia ya kutibu udongo kwa kutumia mvuke ambapo katika toleo hili tutamalizia kwa kuangalia faida zake na njia ya pili ya kutibu kwa kutumia mionzi ya jua. Kutibu udongo kwa kutumia mvuke ni njia ambayo hutumika kwenye kilimo cha ndani na cha nje ili kuondoa na kuua masalia ya magugu, bakteria na…
Fahamu kilimo cha ngolo jinsi kinavyofanyika unufaike
Ngolo ni kilimo cha asili kwa jamii ya wamatengo, ambao ni wakazi wa wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma. Kilimo hiki kinahusisha uchimbaji wa vishimo vyenye mita moja za mraba, na kimo cha sentimeta 40-50. Aina hii ya kilimo, kinafanyika kwenye maeneo yenye mwinuko mkali. Udongo wa maeneo haya una asili ya ulaini hivyo ni rahisi kutengeneza ngolo. Hatua za kutengeneza…
Iliki: Mkombozi wa uchumi wa familia
Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani. Iliki hutumika kama viungo kwenye chakula na pia kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mmea wa iliki ni mfupi na unatoa matunda kwa miaka mingi. Aina za iliki Kuna aina mbili za iliki, ambazo ni: Malabar-Aina hii huzaa kwa kutambaa ardhini na matunda yake ni madogo madogo.…
Uandaaji na uoteshaji wenye tija wa miche ya vanila
Vanila ni zao la biashara ambalo asili yake ni mexico zao hili limekua likilimwa na kuzalishwa huko mexico, marekani na bara Hindi kwa karne nyingine. Hivi sasa, zao hili linalimwa maeneo mengi barani Afrika ikiwamo nchi ya Tanzania, japo kwa uchache kutokana na ugumu wake wa kulizalisha, ingawa bei yake ni kubwa sana na wakulima waliofanikiwa kuzalisha wamekuwa wakipata kipato…
Epuka haya ili usipate hasara katika kilimo
Kwa siku za nyuma, takwimu zilionesha kuwa 80% ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo jambo ambalo kwa sasa inaonekana idadi yao kupungua na kufikia 60%. Hii huenda ikawa ni kutokana na hasara zinazopatikana kwenye kilimo. Hasara katika kilimo zimekuwa ni jambo kubwa ambalo linasumbua vichwa vya wakulima wengi ndani na nje ya Tanzania. Hasara hizi huweza kusababishwa na mambo mengi sana…
Sindika machungwa kuepuka hasara na upotevu usio wa lazima
Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa sana kwa wingi katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Mwanza. Zao hili ni la chakula na biashara. Ikiwa huu ni msimu wa machungwa, wakulima hawana budi kujifunza namna mbalimbali za kusindika zao hili ili kuondokana na upotevu unaotokana na wingi wake na kukosekana kwa soko…
Gliricidia: Mti wenye faida lukuki kwa mkulima
Gliricidia ni mti ambao kisayansi hujulikana kwa jina la gliricidia sepium ambao hutumika kwa ajili ya mbolea au kurutubisha ardhi. Mti huu wa gliricidia ni jamii ya miti ya malisho ambayo majani yake hutumika kurutubisha udongo na kulishia mifugo hasa katika kipindi cha ukame. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kumudu kuzalisha wakati wa kiangazi pamoja na kudumisha hali…
Fahamu kuhusu mazao funika (Cover Crops) na faida zake katika kilimo
Mazao funika ni aina ya mazao ambayo huoteshwa ili kufunika udongo na kwa lengo la kuongeza rutuba ya udongo na kuzalisha chakula na malisho. Mazao funika huoteshwa wakati wa kiangazi au huoteshwa pamoja na zao kuu wakati wa msimu wa kulima. Mazao haya huweza kuachwa kuendelea kuota katika msimu wote wa mazao mseto au yanaweza kungolewa na kuachwa juu ya…