Tafsiri rahisi ya magonjwa ya mimea ni hii: Ni kuwepo kizuizi, au usumbufu fulani unaosababishwa na magonjwa au viumbe fulani kusababisha vichocheo vya ukuaji wa mimea kutokufanya kazi katika hali yake ya kawaida. Kutokana na sehemu ya mmea kupata usumbufu huo, seli za mmea zinaweza kufa au hata kusababisha mmea kufa kabisa. Jambo hili kwa kawaida husababisha kuathirika kwa kiwango…
Kilimo
Faida za kufunika udongo kwenye kilimo hai
Ni kwa namna gani udongo unaweza kufunikwa wakati wote, wakati shughuli nyingine zinaendelea kwenye udongo huo huo? Hili ni swali muhimu wanalojiuliza wakulima wengi. Hii inategemeana na utunzaji na aina ya shughuli zinazofanyika kwenye udongo huo, na kama shughuli zenyewe zinafanyika kwa kutumia mikono au mashine. Moja ya shughuli ambazo zinasumbua udongo kwa kiasi kikubwa ni kulima kwa kutumia plau.…
Tumbukiza ni mbinu inayofaa katika eneo ambalo ni kame na lisilokuwa kame. Ni mbinu ya kuhifadhi maji, na kutoa mavuno mengi zaidi. Ni mbinu ambayo imepokelewa kwa kiasi kikubwa na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka sehemu ambazo wana eneo dogo kwa ajili ya uzalishaji wa malisho. Ni ufumbuzi ambao umeonekana kuleta ongezeko la uzalishaji wa matete kwa asilimia 20…
Magonjwa na wadudu wanaoshambulia tikiti maji
Nimekuwa mkulima wa matikiti kwa muda mrefu, ila bado suala la wadudu na magonjwa yanayoshambulia zao hili ni tatizo kwani hubadilika badilika. Naomba kufahamu wadudu na magonjwa yaliyozoeleka. Mduma Hiza wa Mkuranga Pwani. Katika jarida hili toleo la 10 Januari 2013, tulichapisha makala iliyoeleza vizuri namna nzuri ya uzalishaji wa tikiti maji. Hii ilijumuisha hatua zote muhimu kuanzia utayarishaji wa…
Kilimo mseto na utunzaji wa mazingira
Mara nyingi wafugaji wa mbuzi na hata wale wa wanyama wengine huendesha pia shughuli za kilimo. Katika mashamba yao ya mazao huotesha pia mimea ya aina nyingine, hii ikiwa ni pamoja na miti. Kilimo mseto ni mfumo wa kilimo wa kuchanganya miti na mazao katika shamba moja. Miti sahihi kwa kilimo mseto humnufaisha mfugaji kwa njia nyingi. Miti hiyo huweza…
Madhara yatokanayo na uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO uchafuzi wa mazingira husababisha takribani vifo milioni saba (7) kila mwaka, na kusababisha ulemavu kwa watu wanaoishi na magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa hewa. Nini sababu za uchafuzi wa hali ya hewa Uchafuzi wa hewa husababishwa na gesi na chembechembe zinazoruhusiwa kuingia angani kupitia shughuli mbalimbali za kibinadamu. Miongoni mwa shughuli…
Uzalishaji wa kilimo hai (TAZAMA VIDEO)
Mazao ya kilimo hai Kilimo hai ni aina ya kilimo ambacho hakitumii mbolea wala dawa za viwandani katika uzalishaji wake wa mazao. Mazao yanayozalishwa kwa kutumia kilimo hiki huwa na bei ya juu sana kutokana na kuwa ni salama kwa afya ya mtumiaji. Mazao hayo hayana madhara ya muda mfupi wala mrefu hivyo mtumiaji hana hofu kupatwa na magonjwa.
Wafahamu nzige na jinsi ya kuwadhibiti
Nzige huvamia bustani, shamba na ana uwezo wa kuharibu vibaya kabisa. Katika (matukio mengi) nzige hudhibitibiwa na viuatilifu ambazo ni kemikali sumu za kuua wadudu, ambazo si rafiki na mazingira kwani vinauwezo wa kuua viumbe wengine, pia hatari kwa binadamu. Kutumia hatua mbadala na asili kusaidia kudhibiti idadi yao ni vema. Nzige wa jangwani ni miongoni mwa wadudu wa aina…
Udhibiti wa wadudu kwenye zao la mihogo
Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu. Kilimo cha zao la mhogo, kama ilivyo kwa mazao mengine ya mizizi, kinazongwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wadudu na magonjwa ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiasi cha mavuno,…
Uvunaji na uhifadhi bora wa mazao ya nafaka
Nafaka mbalimbali ambayo ni mazao makuu ya chakula na kibiashara hapa nchini kama vile mahindi, maharage, mikunde mara nyingi wakulima hupoteza hasa wakati wa mavuno kutokana na uvunaji usiokidhi viwango pamoja na uhifadhi duni. Ukiwa huu ni msimu wa mavuno katika maeneo mbalimbali nchini, Mkulima Mbunifu inatoa rai kwa wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni sahihi za mavuno ili waweze kupata…